Sakho avuka kiunzi tuzo CAF

Sakho avuka kiunzi tuzo CAF

mshale21

JF-Expert Member
Joined
Apr 8, 2021
Posts
2,126
Reaction score
5,068
Nyota wa Simba, Pape Osmane Sakho anainyemelea tuzo ya goli bora la mwaka Afrika baada ya bao lake alilofunga dhidi ya Asec Mimosas katika Kombe la Shirikisho Afrika, Februari 13 mwaka huu katika Uwanja wa Benjamin Mkapa kupenya mchujo wa mwisho na kuingia katika kinyang'anyiro cha mwisho kabla ya tuzo zitakazotolewa leo huko Rabat, Morocco.

Katika orodha ya mwisho iliyotolewa jana na CAF baada ya mchujo wa kupunguza idadi ya wanaowania tuzo hizo, Sakho amebaki katika kinyang'anyiro cha goli bora la mwaka akiwa sambamba na Gabadinho Mhango wa Malawi na Orlando Pirates pamoja na Zouhair El Moutaraji wa Morocco na klabu ya Wydad Casablanca.

Kiungo huyo mshambuliaji wa Simba, amewapiku Adama Congo (Burkina Faso), Ben Malango (DR Congo), Ellyes Skhiri (Tunisia), Haithem Layouni (Tunisia), Keitumetse Dithebe (Botswana), Sanaa Massoudy (Morocco) na Youssouf M'Changama (Comoro).

Sakho alifunga bao hilo kwa staili ya tiktak akiunganisha kwa mguu wa kulia krosi iliyopigwa na beki wa Simba, Shomari Kapombe aliyepokea mpira uliotokana na kona fupi iliyochongwa na Rally Bwalya.
 
Kila la kheri, top 3 imeisha hiyo.

Hakosi hla ya MO energy hapo
 
Kila la kheri, top 3 imeisha hiyo.

Hakosi hla ya MO energy hapo
Screenshot_20220720-184050~2.jpg
Kabisa mkuu, tuendelee ku- vote
 

Attachments

  • Screenshot_20220720-184050.jpg
    Screenshot_20220720-184050.jpg
    58.2 KB · Views: 7
Back
Top Bottom