Salaam zangu zikufikie mjomba daktari

Salaam zangu zikufikie mjomba daktari

Shukrani sana kwa mlioipitia post hii, tafadhari isambazeni ili watu wengi zaidi wasome. Najua watanzania tunapenda vipost vifupi vifupi hasa vinavyomjadili mtu mmojammoja ambavyo kimsingi havileti tija saana na natambua ni wachache tu wanaopenda kufikirisha akili yao wanaweza kusoma. Ukombozi wa fikra huanzia na kutambua kwa nini unahitaji ukombozi,basi kaka dada, mwanaume , mwanamke isambaze post hii kwa kuwa inawalenga watanzania woote, japo mjomba daktari ametumika kufikisha ujumbe! Asanteni

Ingekuwa vizuri kama post hii ingewezwa kuchapishwa kwenye magazeti.
 
OMBI KWA MODERATOR:

Naomba hii post uifanye iwe sticky Kwa sababu matatizo ya yaliyoelezewa hapa Ndio changamoto za kweli zinazowapata watu wanaotaka kuikomboa nchi hii!

Inasikitisha sana kuona mwandishi wa habari ambaye amesoma anatoa habari za kuopendelea serikali Kwa makusudi na kumfanya mtu anayepigania wananchi anaonekana Ndio adui yao. Hii Hali Ndio inayowapata wanasiasa wenye nia ya dhati ya kuikomboa nchi hii.

Tuliwaona wachumia tumbo wakitangaza hata wako tayari hata kuwapiga drs mawe kupitia kwenye tv. Hao Ndio wakija muh2 wakiambiwa walale chini sakafuni Ndio watakumbuka maneno yao. Kuna mwana JF ashatembelea wodi za MOI muh2? Wagonjwa wamelala hadi kwenye corridor inayotenganisha wodi na wodi!

Nyie wote mliohongwa ili muwachafue drs serikali inawatumia Kama condom, ambayo ukishaitumia unaitupa!!!
 
Ingekuwa vizuri kama post hii ingewezwa kuchapishwa kwenye magazeti.
Mwandishi au mhariri yeyote anayependa kuichapisha hii gazetini ni ruksa bora tu kwanza anitumie private message ili nimpe consent kulinda haki ya kiuandishi au intellectual right!
 
Hii post inatakiwa isambazwe iwafikie watu wengi zaidi, ukombozi na tiba ya fikra ndo tunayohitaji kwa sasa watanzia ili tuweze kupata uhuru wa kweli. IWekeeni sticky mods mbona kimya mpaka sasa
 
Hii post inatakiwa isambazwe iwafikie watu wengi zaidi, ukombozi na tiba ya fikra ndo tunayohitaji kwa sasa watanzia ili tuweze kupata uhuru wa kweli. IWekeeni sticky mods mbona kimya mpaka sasa
Mkuu Katambala ruksa kuisambaza katika channel tofauti ilimmradi tu mwandishi apewe credit. Watu wanaweza kukujibu mdomo ila hawawezi kuzuia sautizetu kutoka.
 
acha unafiki we ni mmoja ya waliokuwa wanatutukana mtandaoni eti maadili ya udaktari. Tutakutana labour, Mungu atanisamehe kwa staili ntakayokuwa nafanyia kazi. Sie wajinga,wabinafsi,tusio wazalendo, tulogeuka wanasiasa tumekubali. Kuna kazi nyingi nilikuwa nazifanya kwa upendo wa watanganyika wenzangu kumbe mnatuenjoy tu.
Pal, usimlipizie mjinga kwa ujinga.... waliotukana fani wanajijua, wanaumia kimya-kimya na huna haja ya kuonyesha hasira kwa sasa, unawajua, watakuja, utawakumbusha halafu utawatibu, wwatapona ila watabaki na majuto na maumivu ya moyo miaka nenda rudi

Kuna kisa cha ukweli cha mama mmoja mwenye nyodo sana, alikandya watu kwa kuangalia sura, kudhalilisha, akapata ujauzito, akaenda labor, akakutana na dokta ambaye alishamdhalilisha, akagoma kuzalishwa nae, basi wauguzi wote nao wakampisha, akaishia kuzalia chini, na alilazimika kuomba huruma, msaada na msamaha kwa ujumla... NINA IMANI ANA MAJUTO MAREFU

barua ya mjomba nitaisevu!! nitampa credits na nitairusha

ILA WATANZANIA SOMENI KITABU CHA SINDANO INAYOVUJA
 
Kuna kiongozi mmoja wa siasa alishawahi kusema tumerogwa lakini ukweli ni kwamba watanzania tuna tatizo kubwa la kifikra na kimtazamo.ovyo kabisa ukombozi kuja ni shida kwelikweli.

Lakini wachache lazima tufunge mkanda kuyaleta mabadiliko better few but better ila madaktari wameboa sana kwani yote waliyokuwa wanafanya sasa yamekuwa hayana maana kwa kurudi kwao nyuma.

Hivi mapinduzi yanatazama sheria wapi umesikia? Mkiamua kufanya kweli fanya kweli haijalishi mnavunja sheria au la sasa huko ni kubip maendeleo. Sijajua ni woga au baadhi wameshapewa kidogo wakatulia.

Halafu hakuna mgomo iliyowahi kufanikiwa ikiwa wagomaji hawana ushirikiano na vyombo vya habari ndio vinaua kabisa kwani wanatangaza kuwa hawa hawajagoma hawa wamegoma nini hiki?
 
Mtulumbi kwa Mara kwanza umenifanya nitoe machozi,yametutokea mengi lakini shukrani ya watanzania ni kututukana niko pembeni na mjomba,tumewasemehe lakini hatutasahau waliotukashifu kwenye huu mgomo.
invinsible nakuomba uweke sticky

Pole mkuu lakini kumbuka wengi wetu huendeshwa na ushabiki na si uhalisia wa mambo. Lakini ipo siku wataona ushabiki pia hauna tija mungu ibariki Tanzania na wafunue wananchi wake.
 
na hii serikali inapaswa kufundishwa adabu japo wananchi wake wamekuwa hawawezekani lakini naamini ipo siku kitaeleweka tu katika tanzania yetu. mungu atuongoze.
 
Jamani kama kuna wahariri hapa wameiona hii thread hebu tunaomba muichukue mchapishe kwenye magazeti yenu watanzania wapate elimu. hili ni darasa la kutosha.
 
Back
Top Bottom