Salad ya kuku (chicken salad)

Salad ya kuku (chicken salad)

ameline

JF-Expert Member
Joined
Jan 8, 2013
Posts
2,292
Reaction score
1,151
[h=3]SALAD YA KUKU (CHICKEN SALAD)[/h]
Leo nina waletea salad ya kuku.
Kama unavyoona pichani nina vitu vifuatavyo
1.chicken breast(nyama ile ya eneo la kifuani la kuku)
2.maharage machanga
3.mahindi machanga kabisa.
4.Hoho za njano,nyekundu na kijani japo haipo pichani
5.Karoti
6.Broccoli sijui kiswahili chake
7.Squash hizo zinazofanana na matango
8.Kitunguu maji

MATAYARISHO NA UPISHI WENYEWE
Unachukua vipande vya kuku unaviosha vizuri na kuvitia ndimu na tangawizi kisha unachemsha kwa dk 20 maana ni laini sana na rahisi kuiva.Unapochemsha weka chumvi kiasi.Zikiiva unaipua unaweka pembeni.Zikiwa pembeni lile joto ndio unatumia kuivishia kitunguu inamaana hapa ndio utaweka kitunguu maji.

Hakikisha mboga mboga zako umeziosha vizuri kwa maji ya uvugu vugu.Kisha zikate kate weka kwenye sufuria zote kwa pamoja.Baada ya hapo chemsha kwa dk 5 tu ili usiiiue ile kijani lakini zinakuwa zimeiva.Usisahau kuweka chumvi wakai wa kuchemsha.
Ipua na weka kwenye bakuli halafu chukua ile kuku kata vipande vidogo vidogo au vikubwa itategemea unapenda vipi.Changanya vizuriiii na inakuwa tayari kuliwa.Unaweza kuongezea ndimu kidogo au veniger itategemea unapendaje.
Ikiwa bado haijapoa unainyunyizia olive oil kwa juu na unaichanganya vizuri.

Pia unaweza kununua jiko maalum la kusteem mboga mboga,nyama,samaki,kuku kwa mvuke wa maji.Yapo yenye muonekano tofauti tofauti mfano ni kama hili.

Try it! and enjoy it!
 
Sasa hiyo Broccoli ndo ikoje inawezekana naijua kwa kuiona.
 
lol,,,,pia waweza nyunyiza kidogo black pepper powder....ama oregano leaves (kadiri ya ladha unayoitaka) wallahi ni taaaaaaam!
 
Sasa hiyo Broccoli ndo ikoje inawezekana naijua kwa kuiona.
iko kama cauliflower ila yenyewe ni ya kijani, na ni nzuri kwa afya yako. na huyo kuku akiwa wa kienyeji ni powa sana hiyo saladi . yamyam.
 
Nzuri, je unaruhusiwa kushread hizi kuku ikiwa hupendi big pieces
 
Sasa hiyo Broccoli ndo ikoje inawezekana naijua kwa kuiona.

mkuu broccoli iko hivi pichani
images


Mumie ameline asante kwa hii menu...
 
ameline hiyo unaongezea na Mayonise......utajilambaje sasa
 
Last edited by a moderator:
Powa sana ila naona kama umetumia hayo makuku ya kidhungu....ndiyo hayo malaini....wale wetu wenye ladha wanaokula mawe na kokoto hizo dk ni chache sana. Ila kwa ujuzi wangu, ukiwachemsha kwa kutumia vinegar baada ya kuwatoa ngozi wanaiva vizuri na haraka !
 
Back
Top Bottom