Watanzania tuna tabia ya kumheshimu anayetuhesimu, na tunamdharau anayetudharau, wale wakenya na mazungu makanjanja wanaosema serengeti, mlima kilimanjaro, diamondplatnums ni wa kwao sisi tunawadharau lakini VICTOR WANYAMA tunamheshimu saaana kwa sababu naye anawaheshimu watanzania na kutambua umajumuhi wa Afrika mashariki, hana unafiki kama walivyo wakenya wengi, anapapenda Tanzania na kila likizo lazima aje kutusalimia ndugu zake, huko alipo anawakilisha vyema waafrika na wana afrika mashariki kwa kipaji na tabia njema asiye na skendo za kijinga. Kwa nini tusimheshimu na kumpa mtaa?
Tanzania tuna asili hiyo ya kumpa mtu jina la mradi mkubwa pale tunapomheshimu,barabara zetu zote zina majina ya wapigania uhuru wa kwanza akiwemo mzee JOMO KENYATTA, Hospitali zote zina majina kwa heshma ya viongozi na watu maarufu Afrika. Huko Kenye sijawahi kufika na mlivyo wabinafsi kivyenuvyenu sidhani hata kuna mradi wowote mlioupa hata jina la mpigania uhuru aliyechelewesha maendeleo ya watu wake ili kuhakikisha Afrika nzima ipo huru ikiwemo Kenya nazungumzia MWALIMU NYERERE?