Habari Wakuu,
Salama Jabir ni miongoni mwa mastaa wa kike wachache waliofanikiwa kujenga heshima hasa kwenye tasnia ya habari na mwenye uwezo mkubwa sana wa kufanya mahojiano na watu wazito na mwenye uelewa wa aulize nini na asiulize nini kwa mtu anayemfanyia mahojiano
Wanahabari wengi wa Tz wanakosa weledi wa kuuliza maswali hivyo kumfanya muhojiwa asipate nafasi ya kufikisha vitu vingi kwa wanaomskiliza. Kwa mfano, hivi karibuni Lady Jaydee alifanya mahojiano na Milard Ayo kwenye Amplifier na pia alifanya mahojiano na Salama kwenye Salama na ya EATV
Ukifuatilia utaona Salama aliuliza vitu vingi na kwa mpangilio kwa Lady Jaydee na akawa na uwezo wa kufunguka vitu vingi kuliko alivyohojiwa na Milard Ayo. Labda kwasababu ya "usela" wake, vinginevyo Salama Jabir ni miongoni mwa wanawake wenye uwezo mkubwa wa kuhoji na kufanya msikilizaji ashibe taarifa kutoka kwa muhojiwa
Redio presenters wana assignment kubwa ya kufanya kujua namna nzuri ya kupata taarifa kwa watu mashuhuri na sehemu moja wapo ni kujifunza kutoka kwa watu Kama kina Salama Jabir
Ukifuatilia mahojiano yake tangu akiwa na kipindi cha mkasi na sasa "Salama na" utauona uwezo wake wa kutafuta taarifa na kuilisha hadhira taarifa sahihi kupitia mahojiano