Nafaka
JF-Expert Member
- Feb 17, 2015
- 12,154
- 31,246
Jana nimebahatika kutazama kipindi cha Salama Jabir akipiga story na Fatuma Karume.
Wamezungumzia mambo mengi ila mimi kwangu hasa nilichokiona kwa Shangazi ni kwamba ni mtu ambaye hana furaha (ni mtazamo wangu) kutokana na muonekano wake. Na hii ninahisi inasababishwa na mtazamo wake kuhusu mambo yanayoendelea hasa akilalamika sana kuhusu mfumo wa kutoa haki hasa mahakama kuwa hazifanyi kazi kwa haki na kuwa kama mhimili unaojitegemea.
Pia, katika maelezo yake nahisi jambo lingine linalomsumbua, ni kwamba anaona kuna watu wanaonewa wanakandamizwa na hawajui kama wanaonewa wala kukandamizwa bado wanaona kila kitu ni sawa na hata ukiwaeleza hawaelewi unachowaeleza. Hili jambo uwa linawasumbua wengi nadhani Zitto akiwa mmoja kati ya watu ambao uwa wanachambua mambo ambayo wengi uwa hawayaelewi na wala kumsikiliza.
Pia, alijaribu kughusia kuhusu ofisi yao kuchomwa moto japo Salama alimuwahi akamwambia hataki kwenda huko na pia aligusia kuwa kafungiwa kufanya shughuli za uwakili, na akaendelea kuwa anaishi kwa kufanya shughuli za arbitration huko Uingereza na ni shughuli aliyokuwa akiifanya hata kabla hajaanza kufanya masuala ya uwakili Tanzania.
Ilikuwa interview nzuri nilipata kumfahamu zaidi huyu shangazi. Mungu ampatie maisha marefu huyu mwanamama.