Salama vs Zamaradi tukate mzizi wa fitna leo

Zamaradi yuko bora sana
 
Wote wabovu kabisa..

Huyo Zamaradi hajui hata amchague nani amhoji ..yeyote anae trend insta ..wanakuja kumhoji..Mara Gigi money mara Amber Rutty..

Watu wa maana hawafanyiwi interview..


Salama ndo kabisa.. maswali ya kijinga kabisa

Mkuu itoshe tu kusema maudhui ya vipindi tajwa sio mapendeleo yako

Vipindi kama hivi huwa tunasikilizaga kufurahi na kuburudika baada ya kutoka kuangalia Kasongo Hour, Dk 45
 
Hili swali linamkosea Salama Jabir heshima yake aliyojijengea kwenye tasnia tangu planet bongo huko.
Ajabu kunawatangazaji wengi wazamani na upcoming wanasound kama Salama na si Zamaradi.
 
Salama ni zaidi ya Zamaradi..ingawa Salama ana mapungufu yake kwenye kipindi chake kuna aina ya watu anaowaita unategemea kuna maswali atawauliza ila hawaulizi..sijui kwa sababu ni rafiki zake au mfano rejea alivyomwita JK hakuumuliza hata swali lolote kuhus kipindi chake alivyokuwa Rais.
Zamaradi naona kipindi chake kimekaa kimbeambea sana akisikia mtu anaskendo basi huyo kamwita kumuhoji ndio maana kuna kipindi alishawahi kufungiwa baada ya kumwita shoga kumfanyia interviw, lingine production yake ipo low sana sauti haisikiki vizuri kabisa hata mfumo wa maswali anayouliza kama anaropola tu.
 
Tz hakuna kipindi chenye maswali kama ya hardtalk
So sad
Sio kwamba watu hawapendi kuuliza hard questions , bali politician Wana limit namna watakavyokuwa treated kwenye media .
Uliangalia kabudi alivyokuwabanaulizwa maswali na zuhura yunus wa bbc ? That's what happens wanapokosa kubebwa na media.
 
Salama nae hamna kitu kwenye maswali gan aulize anauliza ujinga sometimes anaacha vitu critical hadi unashangaa....nadhan sabab anakuaga na ile hali watazamaji wamjue anaushkaji na anaehojiwa sijui ndo kujipendekeza ama maniaje
 
Salama yupo biased kwenye kuchagua nani amhoji.

Bado hafanyi utafiti wa kutosha kuhusu mtu anayemhoji. Kuna maswali ungetegemea lakini hayatokei. Ugonjwa wa wandishi wengi Tz. Kuna viashiria vya self censorship. Again, ni tatizo la wengi.

Audience ya Salama inaweza kuwa yenye exposure zaidi kuliko ya Zama.

Pamoja na shortcomings zake, Salama kiasi ni bora kuliko Zama.
 
Binafsi wote nawakubali sana, tofauti zao ni hizi, Salama ni mtoto wa mjini sana na anaonesha umjini wake sana kwenye interview but pia anajua sana namna za watu, alivyo muhoji Charles Hilary na Jakaya Kikwete nilizo ona heshima zake kwao, kwa Charles ukiachilia mbali kwamba wanatoka nae Zanzibar but yeye Salama ni rafiki wa mtoto wa Charles so heshima ikawa mara 2, Zamaradi shule imekaa zaidi kichwani but all in all, they are all the best interviewers.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…