Salamu Hii Ya Vijana kwa Watu waliowazidi umri ni Halali?

SHIEKA

JF-Expert Member
Joined
Dec 20, 2011
Posts
8,240
Reaction score
4,265
Wakati fulani nilimsikia kijana mmoja akimsalimu mzee wa makamo kwa kumwambia "Heshima zako mzee" Nilifikiri huyo kijana hakuwa mtanzania kwa sababu huku tanzania tunajua namna ya kumsalimu aliyekuzidi umri.
Ila juzijuzi nilimsikia mtangazaji wa kituo kimoja cha tv- startv - akimsalimia mzee wa makamo: "Heshima zako mzee" naye mzee akajibu, asante.
Nikajiuliza: Je vijana siku hizi wanaanza polepole kubadili salamu tuliyoizoea ya Shikamoo?
Je ni mwelekeo ya salamu mpya kwa siku zijazo?
 
shikamoo ni salam ya kitumwa waarabu walikuwa wakiwasalimia kwa amri kali wa watumwa wao enzi za sultan waliwaambia SHIKAMBOO
Unamtetea huyo kijana.Je wewe binafsi ukikutana na mtu aliyekuzidi umri unamwamkia Heshima zako mzee?
 
Wakati fulani nilimsikia kijana mmoja akimsalimu mzee wa makamo kwa kumwambia "Heshima zako mzee" Nilifikiri huyo kijana hakuwa mtanzania kwa sababu huku tanzania tunajua namna ya kumsalimu aliyekuzidi umri.
Ila juzijuzi nilimsikia mtangazaji wa kituo kimoja cha tv- startv - akimsalimia mzee wa makamo: "Heshima zako mzee" naye mzee akajibu, asante.
Nikajiuliza: Je vijana siku hizi wanaanza polepole kubadili salamu tuliyoizoea ya Shikamoo?
Je ni mwelekeo ya salamu mpya kwa siku zijazo?
Language is not static bt us dynamic
 
Language is not static bt us dynamic
So you are telling us to accept this new greeting of "Heshima yako mzee!" because it is evolutionary greeting brought by dynamism of language?
I have a feeling it will be frowned upon by senior members of our society.
 
Shikamoo ni uxenge sisi nyumbani kwetu hamna hiyo kitu hata mama yangu sijawahi kumwambia shikamoo, na hiyo salamu ndo imewapumbaza watanzania kujiona wako chini na hawawezi kitu, kwani ukimwambia mzee mambo vipi itakua umemkosea adabu?
 
Mkuu naweza kukwambia shikamoo na nikawa sikuheshimu vilevile...what am trying to say is shikamoo haidefine heshima .
Hivyo basi heshima zako mzee ni sawa tuu! "Ninavyofikiri mimi"
 
Mimi kwa mabinti wanaoniamkia shikamoo sipendi kabisa.kwani wanataka kuninyima nini?
 
Shikamoo ni neno la kiarabu lina maana ya Niko chini ya miguu yako. Nadhani kipindi cha utumwa ilikuwa ni lazima umwambie Hivyo mtwana hata kama humuheshimu. Binafsi sidhani kama kuna uhusiano kati ya shikamoo na heshima,wengi ninaowaheshimu siwaamkii shikamoo
 
Upuuzi ni kumwambia mtu shkamoo, hio salamu binafsi naiona ya kipuuzi hata baba yangu mzazi tu siwezi msalimia shkamoo.

Shikamoo ni uxenge sisi nyumbani kwetu hamna hiyo kitu hata mama yangu sijawahi kumwambia shikamoo, na hiyo salamu ndo imewapumbaza watanzania kujiona wako chini na hawawezi kitu, kwani ukimwambia mzee mambo vipi itakua umemkosea adabu?

Mkuu naweza kukwambia shikamoo na nikawa sikuheshimu vilevile...what am trying to say is shikamoo haidefine heshima .
Hivyo basi heshima zako mzee ni sawa tuu! "Ninavyofikiri mimi"

Mimi kwa mabinti wanaoniamkia shikamoo sipendi kabisa.kwani wanataka kuninyima nini?

heshima yako Mzee imetulia haina tatizo.mbona kiaskari askari ata kama Mzee mtu mzima unamwambia jambo afande?

Shikamoo ni neno la kiarabu lina maana ya Niko chini ya miguu yako. Nadhani kipindi cha utumwa ilikuwa ni lazima umwambie Hivyo mtwana hata kama humuheshimu. Binafsi sidhani kama kuna uhusiano kati ya shikamoo na heshima,wengi ninaowaheshimu siwaamkii shikamoo
Wana JF! Zipo dalili kubwa na za wazi kabisa za salamu ya "Shikamoo"kutupiliwa mbali siku si nyingi.Wazee wataanza kulalamika sana kwamba twawakosea adabu.
 
Hakuna kitu nachukia kama kijitu nimekizidi umri kinisalimie 'habari yako'. Afadhali hata hiyo 'heshima yako'
 
Back
Top Bottom