Salamu kutoka Marekani: Nimeinjoi disco la kimya kimya

Salamu kutoka Marekani: Nimeinjoi disco la kimya kimya

Prof Janabi wa JF

Senior Member
Joined
Jul 7, 2023
Posts
165
Reaction score
450
Hili suala la mimi kuwa Marekani mvumilie tu. Nimetoka mbali kama nilivyoeleza uzi uliotangulia. Basi bwana leo mzee wenu nikaambiwa kuna disco la kimyakimya sehemu(Silent disco). Nikasema ngoja nikaone linakuwaje.

Nikaenda mzee wenu, kweli kufika pale naambiwa nijisajili kisha nikapewa headphones, nikaambiwa kuna channel tatu za kusikiliza, kwa hiyo nachagua. Yaani madj wako watatu, kwa hiyo utaamua unataka blues, pop au magoma mengine. Nikasema Tawile!.

Nikavaa headphones, nikaweka sauti hadi mwisho, aisee nimeriungurumisho uno la hatari mzee wenu. Lile uno ni uno kuliko la Harmonize. Nikawa na badili chanel mara kwa mara kutafuta radha za Tz, mara paap nikapata radha za Afrika, aisee, hizo shakushaku nilizozikata pale watu wote wakaniona ni bonge la dancer. Nilipiga shakushaku, nikarudi home nikaweka kiduku, nikahamia kwenye kibega, ngororo, mangumangu, asankolo, malewa, shororo, hadi azonto. DJ akanipeleka sauzi kwenye amapiano. Tena uzuri amapiano nilishajua ile staili ya macho kuweka kama unakufa huku midogo unachezeshachezesha. Nilicheza Amapiano kuliko Costa Tich.

Oya disco la kimya kimya unyama sana... angali moja ya video niliyorekodi watu wakiburudika.


Najua nyumbani tayari asubuhi saa hizi, mimi ndio narudi kulala ni usiku sana now, ila nimeona nije kutamba kidogo
 
We ndo yule jamaa ulikuaga sweden?? Kuna jamaa humu alienda sweden alikua anatu update kila siku, akipanda bus picha akienda popote picha hata begi alilotoka nalo tz alituma picha...... Ndio wewe???
 
Hao wahudhuriaji mbona kama ma 'mental '..wazima kweli haoo
 
Back
Top Bottom