Prof Janabi wa JF
Senior Member
- Jul 7, 2023
- 189
- 490
Habari zenu ndugu zangu! Habari zenu tena!
Nimeshiriki kuangalia applications kadhaa za watu kutoka Afrika kuja US hasa wanaotaka kuja aidha kusoma au kufanya exchange program. Jambo kubwa ninalojifunza ni kuwa watu wa huku mbali na mambo mengine wanaangalia sana "reference letters" au zile barua za udhamini. Namfahamu mtu mmoja ambaye alihangaika kupata PhD kwa miaka zaidi ya 10 kwa kuwa waliokuwa wanamuandikia reference letter walikuwa aidha wanachelewa kuandika au wanaandika hovyo.
Kuonesha watu wako serious kwa sasa reference letters huwa zinahitajika kwenye portal ambapo unaweka email ya anayeku-refer yeye atapokea link ili kuandika kuhusu wewe. Mara nyingi huwa wanapewa wiki mbili za kuandika. Moja ya kitu katika hili lazima uangalie mtu unayemtumia kama reference, usipende kutumia hizi email za public, kama ni academic referee hakikisha una email ya @chuo.ac.tz kama ni professional referee, please chagua ambao nao wana email zisizo za public. Hizi zinaongeza imani, maana watu walikuwa na kawaida ya kuunda email ili kujiandikia reference.
Watu wengi hawapendi kuandika, hivyo hata wakitumiwa email huwa wanawaomba candidates kuandika barua ili wao watume tu. Kazi hii ni ngumu, hasa candidate akihitajika kuwa na referee zaidi ya mmoja yaani kutofautisha content kunakuwa na ugumu. Hata hivyo kaa hapa tuendelee na somo.
Makosa ya barua nyingi
Baadhi ya watu(including professors) mara nyingine wanaandika " Namjua huyu jamaa, alikuwa mwanafunzi/mfanyakazi wangu mpokeeni ni mtu mzuri". Hii barua inaonesha kuwa huyu referee amekukataa. Na inapokuwa hivyo hautakubalika.
Majigambo yasiyo na ushahidi "Huyu jamaa ni mfanyakazi mzuri sana. Kwa kweli sijawahi kujuta tangu kumfahamu nimefanya naye kazi vizuri. Napendekeza azingatiwe kwenye nafasi hiyo" Barua kama hii pia haina uzito.
Makosa ya barua ni kutoonesha uhusiano na hali ya kumfahamu mtu kiundani na kumsifu mtu kwa ushahidi.
ZINGATIA
Andika barua kwa kuonesha unamjua Candidate na unajua anachokifanya. Pia onesha unaijua taasisi/kitu alichoomba. Hii inaonesha kuwa mnamawasiliano mazuri.
Onesha muda na kitu kilichowanganisha, unaweza kutia chumvi kwa kuonesha bado mnawasiliana hata kama hamjatafutana kwa miaka dahari.
Kwenye kumsifu mtu tumia mifano, hasa kazi mlizofanya pamoja. Andika kiingereza kizuri aisee, jitahidi ndugu yangu andika barua, kisha tupa kwenye AI ikurekebishie English yako ya kuunga unga.
Mfano wa Barua Nzuri ya reference
Let: Taasisi ni Havard, nafasi inayoombwa ni Research Assistantship ktk mambo ya Afya, tufanye mimi ni prof kweli ambaye namuandikia Barua ndugu Nungunungu.
Nina furaha kuandika barua ya kumpendekeza Nungunungu kuwa msaidizi wa tafiti ya masuala ya Afya ktk Chuo cha Havard. Havard inafahamika kwa tafiti nzuri ambazo zinasaidia sio tu Marekani bali hata nchi zinazoendelea kama Tanzania. Tafiti ya prof Janabi akiwa Havard ni mmoja wa tafiti iliyosaidia sana katika kuboresha lishe kwa watoto huku Tanzania. Hata mimi nimeitumia sana kufundishia wanafunzi wangu huku Tanzania.
Nimemfahamu Nungunungu tangu mwaka 2001 alipojiunga na chuo cha JF kwa masomo ya shahada ya awali. Niliona ari yake ya kujifunza mambo ya afya na nikamshirikisha kwenye baadhi ya projects zangu ili aweze kujifunza zaidi. Baadhi ya project ambazo Nungunungu alishiriki nami moja kwa moja ni pamoja na project ya kupambana na marelia katika vijiji vitano Tanzania, ambapo alienda kama mkusanya data. Kazi yake ilikuwa bora na alionesha umahiri wa kutumia vifaa vya kidigitali na kuwasilisha taarifa ndani ya wakati. Kuonesha mapenzi yake kwa masuala ya afya, aliweza kuweka maandiko kadhaa katika ukurasa wake wa insta kuhusu zoezi lile.
Nungunungu nimefundisha takribani kozi kadhaa, ikiwemo koditomy, tozotomy, Tanzatomy na chawatomy. Kozi hizi alionesha umahiri mkubwa wa kuzimudu na kupata marks zilizomsaidia kufanya vyema kwenye tafiti yake ya kukamilisha masomo yake ya shahada. Tafiti yake ilikuwa bora kiasi cha kuwa published Kizimkazi Journal of science. Mbali na matokeo mazuri Nungunungu ameshiriki katika kazi mbalimbali za Afya ikiwemo kujitolea kuwahamasisha watu mtandaoni kama ilivyo kwenye ukurasa wake(weka link). Pia amejitoleamaeneo mbalimbali ikiwemo JF Hospital ambapo daima watu walimfurahia na kumtangaza vyema hadi alipata tuzo mwaka elfu mbili na nanii.
Nungunungu ni mtu mwenye nia ya kujifunza na kutaka kufanya mabadiliko katika sekta ya afya hapa Tanzania. Nafasi hiyo ya kuwa msaidizi wa tafiti itamfanya kuwa mtu bora zaidi na mwenye matokeo chanya hapa nchini kwetu. Kwania, utashi na ari aliyonayo natambua nafasi hiyo itamfanya awe na nafasi nzuri ya kufanya PhD suala ambalo amekuwa akilizungumza kila wakati nikiwasiliana naye kwa email.
Kwa mambo haya ninayoyafahamu kuhusu Nungunungu, siwezi kusita kupendekeza awe ni mmoja kati ya watu katika nafasi hiyo. Niko tayari kwa kutoa maelezo zaidi kuhusu Nungunungu wakati wowote mkihitaji.
Ndimi
Prof Janabi wa JF
Mkuu wa Upuuzi mtandaoni
[email protected]
Mfano wa Barua ya hovyo
Mimi Janabi wa JF, namfahamu Nungunungu vizuri kwa kuwa nimefundisha, hivyo napendekeza mumzingatie kwa maombi yake ya usaidizi wa Utafiti Havard.
Ndimi
Prof Janabi wa JF
Mkuu wa Upuuzi Mtandaoni
[email protected]
Baada ya maelezo haya, nasign out.
Salamu kutoka kwa Trump, na kwenye moto Los Angeles
Prof Janabi wa JF.