Chakaza
JF-Expert Member
- Mar 10, 2007
- 40,455
- 73,145
Salamu za Kwaresima toka kwa Baba Askofu Bagonza (PhD).
DHAMIRI SAFI, DIRA YA TAIFA
Tuongozwe na Katiba?
Tuongozwe na Mtu?
Tuongozwe na Dhamiri?
Tuongozwe na Chama?
Tuongozwe na Vyombo?
Niliwahi kukumbusha:
Kule kwa jirani, “Hawa walipaza sauti, Wale wakanyamaza. Lakini sasa, kila mwaka wote wanakusanyika kuombea mafuvu na makaburi”.
Tunaingia Kwaresima; na wengine tayari ndani ya mfungo. Yaonekana wengi wana matumaini na vyama kuliko Muumba wanayefunga kwa ajili yake. Lakini ukiviangalia vyama hivi?!
CCM wana kigugumizi sugu. Hawataki kukiri kuwa kuna mambo yalienda vibaya na ndiyo maana Mama akaja na 4R. Hazikutoka mbinguni. Mtangulizi wake aliziandaa bila kujua kwa kuweka mazingira yaliyozizalisha. Bila 4R hizi kutekelezwa, tunaandaa 10R baada ya uchaguzi!
CDM na ACT wana Kwikwi. Wanatembea katikati ya fadhila na haki. Kuna kitu mdomoni; wakitema wanatema utamu (kushiriki uchaguzi); wakimeza wanameza moto (kushiriki wakiwa na uhakika wa kuonewa).
Wote CCM na Wapinzani wanasahau upesi. Tukipuuza ukuu wa katiba hakuna aliye salama. Tukipuuza ukweli kuwa HAKI ndiyo inaleta AMANI hakuna aliye salama. Tunakuza watu wawe na nguvu kuliko sheria, katiba na kuwa na nguvu kuliko taasisi.
Wayahudi (Mayahudi) walimtenda Yesu (Nabii Issa) mambo mabaya ili kumwambukiza kigugumizi na kwikwi. Alikufa kama mhalifu, akawaokoa wahalifu.
Mnadhani njia ya Wayahudi inatufaa sana. Haifai. Kwa nini?
1. Kwa sababu, Kuna watu wako tayari kufanya lolote kumdhuru yeyote asiye na kigugumizi au kwikwi. Wanasema, “subutu muingie barabarani”, “tutawapoteza”, “tutawavunja miguu”, tutawachapa kichapo cha mbwa koko”, nk. Hawa tunao, wanaweza na wamewahi kufanya hayo wanayoapa kufanya. Ni zaidi ya Mayahudi walivyomfanyia Mnazarethi.
2. Hakuna watu wengi walio tayari kufanyiwa hayo ya namba 1 juu. Wako tayari kuvunjika moyo kuliko kuvunjika miguu na mikono. Wako tayari kukata tamaa na maisha na kujiua lakini si kuua au kuuawa. Wako tayari kuibiwa kura lakini si kuiba kura. Watu wema hawa. Wanageuza shavu la kulia pale la kushoto likichoka. Wanamfia nani? Yesu aliwafia wao.
Siku haya makundi 2 yakiungana, (natamani yasiungane), atakayebaki atakosa wa kumzika! Yaani walio tayari kuua wakiungana na walio tayari kufa, tutapata zaidi ya taabu.
Prof. Kabudi kabla hajaokoka aliwahi kutushauri “tusisubiri” wawe wengi.
Mtani wangu anasema tusubiri tumalize uchaguzi.
Walevi walioshindwa kuacha pombe huwa wanapanga kuacha kesho!
Naenda ibadani lakini Bwana anatualika akisema, “Haya Njooni Tusemezane, dhambi zenu zikiwa nyekundu kama damu, nitazisafisha ziwe nyeupe kama theruji ” ( Isaya 1: 18).
Taifa lolote lililostawi hustawi juu ya Ukuu wa Katiba na uongozi ulio na dhamiri safi. Sheria zikikanyagwa, katiba ikahairishwa, watunza dhamiri (viongozi wa dini) tukaugua kwikwi na kigugumizi; Upanga wa Bwana watungoja (Isaya 1: 20).
Kwaresima Njema.