Salamu za Askofu Bagonza kwa Makalla na Wenzake, Sisi Tumeshazipokea. Mwenye Kusikia na Asikie.

Salamu za Askofu Bagonza kwa Makalla na Wenzake, Sisi Tumeshazipokea. Mwenye Kusikia na Asikie.

Ukizisoma kwa umakini ni kama ONYO kwa CCM kuwa yajayo ni mabaya kama wanakomaza shingo.
Neno "wakiungana waliotayari kuua (vyombo vya dola yaani Jeshi na police) na walio tayari kufa (wananchi wanaotaka haki) waliobaki watazikwa na nani? Hiyo ni falsafa kubwa na wasipo ielewa ndio mwisho wao.
TUSIREMBE MANENO.
Hayo ni maoni kama maoni mengine ila hakuna mwananchi mwenye akili timamu akaenda kuandamana mzee chakaza...
 
Hayo ni maoni kama maoni mengine ila hakuna mwananchi mwenye akili timamu akaenda kuandamana mzee chakaza...
Mkuu wangu kipara kipya kwanza habari ya siku!
Mbona unapenda kukariri maisha? Kwanini watu waandamane kama hizo reforms zitafanyika?
Unajua ni kama CCM Inafanya majaribio na uwezo wa watu kwa vile inaanini Jeshi, polisi, mgambo nk ni vyombo vyao kama chama kwa sababu bado mnaongozwa na watu kama Wassira ambao enzi zao ulikuwa huwi katika vyombo hivyo bila kadi ya Chama.
Hivi uchaguzi wa 2019,2020 na 2024 hauwezi kuwapeni RED ALERT kuwa sasa wananchi wamechoka na kufanywa wajinga?
General Al Bashir wa Sudani alisababishiwa kuondoka madarakani na nguvu ya umma iliyoratibiwa na Binti mdogo na moto wake wakashindwa kuuzima sababu ya dharau zao!
Mpaka leo yuko wapi yeye na wapambe wake? Jela anasota.
Askofu Bagoza katumia falsafa kutufundisha hapo kuwa "siku walio tayari kuua na walio tayari kufa wakiungana tutapata shida" ni nani hao?
Tafakari.
 
Mzee Mwenzangu Alhamdulilah majukumu ni mengi ila wewe ndio um-disappear to appear..mimi sijakariri kuhusu maandamano ila kama utarudia kusikiliza hutuba ya lissu amesema atahamasisha na kushawishi wananchi watoke barabarani hata slaa amerudia hiyo kauli sasa ukisema nakariri hapana..bagoza huwa anasema mengi yanayopitia kichwani mwake anachotamani wala hakito tokea nani aache kutafuta pesa yake ya kujenga na kusomesha wanawe akashiriki upuuzi bagoza keshachoka akapambane aonyeshe mfano!
 
Taifa kuwa na watu wajinga kama wewe ni hasara sn
 
Ukizisoma kwa umakini ni kama ONYO kwa CCM kuwa yajayo ni mabaya kama wanakomaza shingo.
Neno "wakiungana waliotayari kuua (vyombo vya dola yaani Jeshi na police) na walio tayari kufa (wananchi wanaotaka haki) waliobaki watazikwa na nani? Hiyo ni falsafa kubwa na wasipo ielewa ndio mwisho wao.
TUSIREMBE MANENO.
SWALI Sasa wataungana lini? Ukilipata jibu utaniita. Nimekaa palee
 
Salamu za Kwaresima toka kwa Baba Askofu Bagonza (PhD).

DHAMIRI SAFI, DIRA YA TAIFA

Tuongozwe na Katiba?
Tuongozwe na Mtu?
Tuongozwe na Dhamiri?
Tuongozwe na Chama?
Tuongozwe na Vyombo?

Niliwahi kukumbusha:

Kule kwa jirani, “Hawa walipaza sauti, Wale wakanyamaza. Lakini sasa, kila mwaka wote wanakusanyika kuombea mafuvu na makaburi”.

Tunaingia Kwaresima; na wengine tayari ndani ya mfungo. Yaonekana wengi wana matumaini na vyama kuliko Muumba wanayefunga kwa ajili yake. Lakini ukiviangalia vyama hivi?!

CCM wana kigugumizi sugu. Hawataki kukiri kuwa kuna mambo yalienda vibaya na ndiyo maana Mama akaja na 4R. Hazikutoka mbinguni. Mtangulizi wake aliziandaa bila kujua kwa kuweka mazingira yaliyozizalisha. Bila 4R hizi kutekelezwa, tunaandaa 10R baada ya uchaguzi!

CDM na ACT wana Kwikwi. Wanatembea katikati ya fadhila na haki. Kuna kitu mdomoni; wakitema wanatema utamu (kushiriki uchaguzi); wakimeza wanameza moto (kushiriki wakiwa na uhakika wa kuonewa).

Wote CCM na Wapinzani wanasahau upesi. Tukipuuza ukuu wa katiba hakuna aliye salama. Tukipuuza ukweli kuwa HAKI ndiyo inaleta AMANI hakuna aliye salama. Tunakuza watu wawe na nguvu kuliko sheria, katiba na kuwa na nguvu kuliko taasisi.

Wayahudi (Mayahudi) walimtenda Yesu (Nabii Issa) mambo mabaya ili kumwambukiza kigugumizi na kwikwi. Alikufa kama mhalifu, akawaokoa wahalifu.

Mnadhani njia ya Wayahudi inatufaa sana. Haifai. Kwa nini?

1. Kwa sababu, Kuna watu wako tayari kufanya lolote kumdhuru yeyote asiye na kigugumizi au kwikwi. Wanasema, “subutu muingie barabarani”, “tutawapoteza”, “tutawavunja miguu”, tutawachapa kichapo cha mbwa koko”, nk. Hawa tunao, wanaweza na wamewahi kufanya hayo wanayoapa kufanya. Ni zaidi ya Mayahudi walivyomfanyia Mnazarethi.

2. Hakuna watu wengi walio tayari kufanyiwa hayo ya namba 1 juu. Wako tayari kuvunjika moyo kuliko kuvunjika miguu na mikono. Wako tayari kukata tamaa na maisha na kujiua lakini si kuua au kuuawa. Wako tayari kuibiwa kura lakini si kuiba kura. Watu wema hawa. Wanageuza shavu la kulia pale la kushoto likichoka. Wanamfia nani? Yesu aliwafia wao.

Siku haya makundi 2 yakiungana, (natamani yasiungane), atakayebaki atakosa wa kumzika! Yaani walio tayari kuua wakiungana na walio tayari kufa, tutapata zaidi ya taabu.

Prof. Kabudi kabla hajaokoka aliwahi kutushauri “tusisubiri” wawe wengi.
Mtani wangu anasema tusubiri tumalize uchaguzi.

Walevi walioshindwa kuacha pombe huwa wanapanga kuacha kesho!

Naenda ibadani lakini Bwana anatualika akisema, “Haya Njooni Tusemezane, dhambi zenu zikiwa nyekundu kama damu, nitazisafisha ziwe nyeupe kama theruji ” ( Isaya 1: 18).

Taifa lolote lililostawi hustawi juu ya Ukuu wa Katiba na uongozi ulio na dhamiri safi. Sheria zikikanyagwa, katiba ikahairishwa, watunza dhamiri (viongozi wa dini) tukaugua kwikwi na kigugumizi; Upanga wa Bwana watungoja (Isaya 1: 20).

Kwaresima Njema.
Sikio la kufa halisikii dawa.
 
Hapa sijaelewa
Wananchi(Wanyonge),,Waliojishibia Hupenda Kuwaita Hivyo Wakiungana Na Wananchi Wenzao Ambao Wamebahatika Kufanya Kazi Katika Vyombo Vya Usalama Na Hao Ndio Hutumika Na Kutumiwa Na Waliojishibia,,Kwa Maono Ya Askofu Uvumilivu Unaishaga Anaona Hatari Kwa Waliojishibia Na Nchi Kiujumla
 
Ukizisoma kwa umakini ni kama ONYO kwa CCM kuwa yajayo ni mabaya kama wanakomaza shingo.
Neno "wakiungana waliotayari kuua (vyombo vya dola yaani Jeshi na police) na walio tayari kufa (wananchi wanaotaka haki) waliobaki watazikwa na nani? Hiyo ni falsafa kubwa na wasipo ielewa ndio mwisho wao.
TUSIREMBE MANENO.
Haya maneno watu waovu wameyasema lakini Tanzania ni salama na itahepuka chokochoko zote na itabaki salama kama ilivyokuwa salama juzi,jana na leo!
 
Back
Top Bottom