Doctor Mama Amon
JF-Expert Member
- Mar 30, 2018
- 2,089
- 2,725
Picha ya Rais Samia Suuhu Hassan akihutubia Taifa usiku wa 31 Desemba 2021
Mheshmwa Rais Samia Suluhu Hassan,
Hotuba yako kwa Taifa wakati tunauaga mwaka 2021 na kuingia mwaka Mpya wa 2022 nimeisoma yote.
Ni nzuri, inaleta matumaini, kuondoa taharuki na kuonyesha ndoto yako kwa ajili ya Taifa katika mwaka unaofuata.
Nakutakia kila la heri katika kutimiza ndoto uliyo nayo kwa ajili ya Taifa letu lenye umri wa miaka ipatayo 60 sasa.
Lakini, napenda kukusihi ufanyie kazi suala moja muhimu kwa Taifa.
Ni kuhusu nafasi ya Kanuni ya 5K's katika uendeshaji wa nchi.
Yaani, naongelea Kupanga, Kutekeleza, Kufuatilia, Kutathmini, na Kuboresha.
Kilichofanyika hadi sasa kuhusu 5Ks:
- Tayari tunao mpango wa Tatu wa Maendeleo wa Taifa wa 2021 hadi 2026, yaani TFYDP-III.
- Tayari tumewasikia mawaziri wakitangaza simulizi za mafanikio ya kisekta na kiwizara kwa miaka 60 wakati ule tulipokuwa tunajiandaa kwa ajili ya kusherehekea siku ya uhuru wa 9 Desemba 1961.
- Tayari Wizara zisizozidi tatu (3) zimetangaza hadharani Mipango Mikakati yake ya miaka mitano (5).
- Wizara ya TEHAMA, chini ya Waziri wa zamani, ilitutangazia Mpango usio kidhi mahitaji ya Wizara na Taifa kuhusiana na nguzo tano za Taifa la Kidijitali, yaani digital infrastructure, digital economy, digital government, digital society, na digital security.
- Bado Wizara ya Fedha haijaweka hadharani mfumo wa Kufuatilia na Kutahmini FYDP-III.
- Bado Wizara zaidi ya kumi na saba (17) hazijaweka hadharani Mipango ya Maendeleo ya miaka mitano ijayo.
- Bado Sekretarieti za Mikoa mingi hazijaweka bayana Mipango ya Maendeleo ya miaka mitano ijayo, yenye kuendana na FYDP-III.
- Bado Sekretarieti za Mikoa mingi hazijaweka bayana Mipango ya Maendeleo ya Mwaka wa 2022, yenye kuendana na FYDP-III
- Bado Halmashauri nyingi hazijaweka bayana Mipango ya Maendeleo ya miaka mitano ijayo, yenye kuendana na FYDP-III.
- Bado Halmashauri nyingi hazijaweka bayana Mipango ya Maendeleo ya mwaka 2022, yenye kuendana na FYDP-III.
- Kutoka na mapengo haya, serikali haitaweza kufanya kazi ya kufuatilia, kutathmini, na kuboresha utekelezaji wa kazi yake katika kipindi kinachoanza jana 01 Januari 2022.
- Kitakachowezekana ni serikali kufanya kazi kwa mujibu wa utaratibu wa "mbele kwa mbele", yaani utaratibu wa zima moto, ambao wakati mwingine huwa unakwamisha mambo.
Maombi kwako Mhe. Rais:
- Katika kikao cha Baraza la Mawazi kijacho uwakumbushe waheshimiwa kutimiza wajibu wao katika suala la 5K bila kuchelewa.
- Kwa kuwa Wizara ya TAMISEMI ndiko serikali inakokutana na umma uso kwa uso, mwagize Waziri Ummy kuandaa kikao kazi na ma-RAS, ma-DAS na ma-DED kwa ajili ya kuweka mkazo katika ajenda ya 5K.
- Na kwa kuwa sasa dunia imo katika Zama za Nne za Mapinduzi ya Viwanda (4IR), mwagize Waziri wa TEHAMA kuboresha Mpango Mkakati wa Wizara yake kwa kubainisha kinaganaga mikakati kwa ajili ya maeneo yafuatayo: digital infrastructure, digital economy, digital government, digital society, na digital security.
Nakusalimia kwa jina la Jamhuri ya Muungano, na kazi iendelee kwa kasi na viwango!
Karibuni kwetu Simbawanga.
Mama Amon,
Simbawanga Mjini.