Saleh Ally vs Edo Kumwembe

MamaSamia2025

JF-Expert Member
Joined
Mar 29, 2012
Posts
14,588
Reaction score
32,361
Wadau nimeona niilete mada hii hapa jamvini kuhusu hawa wachambuzi wa habari za michezo magazetini. Saleh yupo Championi na Edo yupo Mwanaspoti. Je, unavyoona nani mkali zaidi kati yao?
 
Wadau nimeona niilete mada hii hapa jamvini kuhusu hawa wachambuzi wa habari za michezo magazetini. Saleh yupo Championi na Edo yupo Mwanaspoti. Je, unavyoona nani mkali zaidi kati yao?

Saleh Ally sijamfuatilia vizuri labda niseme upenzi wangu uliotukuka wa kusoma gazeti ka MwanaSpoti ndio maana,


Sent from my iPad Air using JamiiForums mobile app
 
Edo Kumwembe ana tabia ya kuongeza chumvi,kwa sisi wazoefu chumvi zake hua zinaleta ukakasi, mfano aliwahi kuchambua kwamba mstaa wetu ni wale ambao huwa na majina yao ambao yanawahusu wao tu hapa alimananisha siyo vizuri staa wenu ati mnamwita MESSI mfano, au Cannavaro ambae ni back wa Italia.

Akatoa mfano Sunday Manara -Computer, halafu akasema Zamayoni Mogela -GORDEN BOY alipewa kama ndio jina lake la kipekee wakati Gorden boy original alikuwa ni Abdullazak wa Accra Hearts of oak ya Ghana, ni alipewa na wapenzi miaka ya 75, sisi kwa Mogella tulicopy na kupaste toka kwa Abdullazak wa Ghana, chumvi za namna hii mimi huwa zinanikela ndo maana dogo huyu simpendi, mala nyingi tu nakamata uwongo.
 

bro shkamoo. wewe basi ni mkongwe kwenye haya mambo
 
Tatizo siyo uchambuzi bali mwanaspoti na championi ni zaidi ya wapinzani.
 
Eddo juu, juuuu zaidi, mtu na akili zako huwezi soma udaku wa champion.
 
Sijawai kutoa hela mifukoni kununua gazeti la champion, hata hivyo Eddo yupo juu.
 
championi nimesahau nimesoma lini...so siwezi sema lolote juu ya huyo saleh Ally...
 
Nadhani tumelinganisha watu wawili wenye uwezo na kazi tofauti japo wote wapo kwenye print media.

Edo ni mchambuzi hasa japo anaongeza 'ladha' zaidi katika uchambuzi wake unaombatana na sanaa huku akiweka wazi hisia na mtazamo wake bila kuweka facts nyingi. Anaonekana anaweza kuwa na kipaji kikubwa sana cha utunzi kama wa hadithi, mashairi. nk.

Salehe Ally namwona kama ni mwandishi zaidi kwa maana ya ripota haswaa, lakini pia ni mtu anayejikita ktk kusahihisha mambo bila kumung'unya maneno. Kwa mtazamo wangu bado hafanyi uchambuzi kwelikweli kwa sababu anaweka hisia zake wazi ktk makala kwa hiyo ile objectivity ambayo ni nguzo muhimu ya uchambuzi inakosekana

Mwisho, lazima tujifunze kutambua na kuthamini upekee na mchango wa kila mtu. Edo hawezi kuwa Salehe na vivyo hivyo Salehe hawezi kuwa Edo. Wote wana uwezo tofauti, vipaji tofauti, mtazamo tofauti na mchango tofauti tofauti ktk fani hii ya uandishi.
 
Napenda aina ya uchambuzi wa edo kumwembe

Salleh ally sijamsoma siku nyingi sana
 

napenda mchangiaji kama huyu badala ya kuleta matusi
 
Nimesoma makala kadhaa za Saleh Ally, ni nzuri na zinafunza kitu. Edo ni kipenzi cha Watanzania wengi lakini sipendi chambuzi zake kwa kwa anaandika khusu mambo ya Ulaya yasiyo na msaada kwetu, na akiandika kuhusu soka la nyumbani anaandika kwa staili ya kunanga.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…