MamaSamia2025
JF-Expert Member
- Mar 29, 2012
- 14,588
- 32,361
Wadau nimeona niilete mada hii hapa jamvini kuhusu hawa wachambuzi wa habari za michezo magazetini. Saleh yupo Championi na Edo yupo Mwanaspoti. Je, unavyoona nani mkali zaidi kati yao?
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Wadau nimeona niilete mada hii hapa jamvini kuhusu hawa wachambuzi wa habari za michezo magazetini. Saleh yupo Championi na Edo yupo Mwanaspoti. Je, unavyoona nani mkali zaidi kati yao?
Edo Kumwembe ana tabia ya kuongeza chumvi,kwa sisi wazoefu chumvi zake hua zinaleta ukakasi, mfano aliwahi kuchambua kwamba mstaa wetu ni wale ambao huwa na majina yao ambao yanawahusu wao tu hapa alimananisha siyo vizuri staa wenu ati mnamwita MESSI mfano, au Cannavaro ambae ni back wa Italia.
Akatoa mfano Sunday Manara -Computer, halafu akasema Zamayoni Mogela -GORDEN BOY alipewa kama ndio jina lake la kipekee wakati Gorden boy original alikuwa ni Abdullazak wa Accra Hearts of oak ya Ghana, ni alipewa na wapenzi miaka ya 75, sisi kwa Mogella tulicopy na kupaste toka kwa Abdullazak wa Ghana, chumvi za namna hii mimi huwa zinanikela ndo maana dogo huyu simpendi, mala nyingi tu nakamata uwongo.
Nadhani tumelinganisha watu wawili wenye uwezo na kazi tofauti japo wote wapo kwenye print media.
Edo ni mchambuzi hasa japo anaongeza 'ladha' zaidi katika uchambuzi wake unaombatana na sanaa huku akiweka wazi hisia na mtazamo wake bila kuweka facts nyingi. Anaonekana anaweza kuwa na kipaji kikubwa sana cha utunzi kama wa hadithi, mashairi. nk.
Salehe Ally namwona kama ni mwandishi zaidi kwa maana ya ripota haswaa, lakini pia ni mtu anayejikita ktk kusahihisha mambo bila kumung'unya maneno. Kwa mtazamo wangu bado hafanyi uchambuzi kwelikweli kwa sababu anaweka hisia zake wazi ktk makala kwa hiyo ile objectivity ambayo ni nguzo muhimu ya uchambuzi inakosekana
Mwisho, lazima tujifunze kutambua na kuthamini upekee na mchango wa kila mtu. Edo hawezi kuwa Salehe na vivyo hivyo Salehe hawezi kuwa Edo. Wote wana uwezo tofauti, vipaji tofauti, mtazamo tofauti na mchango tofauti tofauti ktk fani hii ya uandishi.
Eddo juu, juuuu zaidi, mtu na akili zako huwezi soma udaku wa champion.
Dahna bin zuber mchumia tumbo je?