Salim Abdalla " Try Again" Acha Kuihujum Simba

Orketeemi

JF-Expert Member
Joined
Feb 12, 2013
Posts
5,063
Reaction score
12,866
Siku chache kabla ya pambano la ugenini dhidi ya Asec Mimosas ,, boss mkubwa wa Simba Try Again anasikika akitamba kwamba Simba itasajili Wachezaji wanne wa kigeni mwishoni mwa msimu. Kipigo dhidi ya Asec kilianzia hapo.

Twende taratibu.

Kwa mujibu wa KANUNI za TFF kila Klabu nchini inaruhusiwa kusajili Wachezaji wa kigeni si zaidi ya 12.

Pale Simba tayari kuna maproo 12 ,, nakutajia Chama, Bwalya , Lwanga, Sakho, Kanoute, Wawa, Kagere, Morrison, Onyango, Inonga, Mugalu na Peter Banda.

Kwa maana hiyo ili Simba iweze kusajili maproo wengine wanne italazimika kuwafuta kazi maproo wanne ambao wapo kikosini Kwa sasa. Tim Inaelekea kwenye mechi ngum na muhim then unatoa maneno Kama haya Kwa malengo gani?

Watu wanapambana uwanjani lakin uongoz umetoa ahadi ya kuwafuta kazi Wachezaji wanne wa kigeni mwisho wa msimu. Hii ni nini kisaikolojia Kama si kuwaweka Wachezaji kwenye presha isiyo na msingi wowote?

Nabet Simba anakwenda kuadhibiwa na USGN pale pale kwa Mkapa na kufurushwa mashindanoni.

Tangu kifo cha Comred Hans Poppe ilisemwa pale Simba hakuna tena mwenye uwezo wa kuisogeza timu mbele. Waliowengi walikuwa wanaishi kwenye kivuli cha Hans Poppe.
 
Siku chache kabla ya pambano la ugenini dhidi ya Asec Mimosas ,, boss mkubwa wa Simba Try Again anasikika akitamba kwamba Simba itasajili Wachezaji wanne wa kigeni mwishoni mwa msimu. Kipigo dhidi ya Asec kilianzia hapo....
Mkuuu Punguza Makasiriko, lkn wewe pia siyo Mwanasimba kwa Maombi yako kwamba Mnyama anakuja kufungwa kwa Mkapa endelea kukata Majani ulishe Mifugo yenu huko Utopwinyo.

Simba kuna Kauli yao NGUVU MOJA so usilete chokochoko za Kindezi hapa. Hiyo kauli wenye Simba yao wameiona na wameiskia lkn pako mahala sahihi pa kusemea hilo siyo hapa ulipolimwaga wewe unalo lingine tu.
 
Mkuuu Punguza Makasiriko, lkn wewe pia siyo Mwanasimba kwa Maombi yako kwamba Mnyama anakuja kufungwa kwa Mkapa endelea kukata Majani ulishe Mifugo yenu huko Utopwinyo...
Kuusema ukweli haimfanyi mtu kutokuwa shabiki wa Simba,,.

Pale Simba kuna hujuma za wazi kutoka kwa baadhi ya viongozi Wakiongozwa na Try Again
 
sasa si ndo vizuri mr utopolo ili ufurahi, majinga yanahahakam simba itaingia robo fainali au vipi yaan standard ya simba na matarajio yamekuwa makubwa kuna majitu mengine kuvuka tu round ya awali ni kizungumkuti

Yaani unadhani, mugalu, wawa kagere hawajui kwamba wanaondoka??? yaani ulitaka awapambe vipi sasa, hopeless kama nyie mnaweza kuwapamba kina moloko na chiko ushindi na makambo endeleeni , tarehe 3- 4 saa tatu usiku uje urudio uzi wako huu
 
Ila mashabiki wa Simba ni takataka, wahuni wahuni tu kwahiyo mlitaka simba wa shinde kwa wachazaji hawa wabovu?
jinsi ulivyo boya unadhani tumetolewa siyo? hao asec si walikula tatu hapa mkapa? mbona kama mmestuka simba kufungwa? hamkutarajia siyo?

angalia hawa wahuni mara ya mwisho kuingia makundi utopolo waliofanya, teams zenyewe Gor mahia na Raon unashindwa kushika hata nafasi ya pili
 
Hayo mapendekezo yako ya timu kuhujumiwa mpelekee yule Tetesaikline wenu ili aitishe press Comferance
 
Kwa akili zako unadhani simba hii sawa na ile iliyocheza club bigwa miaka ya nyuma? Halafu nyie nyie ndio mnatakaa matokeo mazuri? Sema nyie mashabiki wa simba akili zenu mnazijua wenyewe watu wa low capacity thinking
 
Ila hata mimi mshamba wa mpira nilijiuliza kwanini kutaja nani ataingia nani atatoka imekuwa mambo ya kutoa notisi kwa wapangaji?

Kiongozi mhusika afanye aliteleza asirudie mbele ya safari.
 
Wachezaji wa yanga wameitwa wangapi team ya taifa au ndio mda wa kuchunga ng'ombe wa mayele
 
Mugalu out
Kagere out
Wawa out
Lwanga out
Lwanga in
Morrrison Out.

Mudi amchukue mmojawapo Kati ya Hawa.
Aziz Ki,Adebayo wa USGN(Japo Ni mbahili na kuwang'oa hao nyota Ni shughuli).Tunahitaji mchezaji wa kuanza kwny mechi na si aina ya kina Morison,Benchi sana pesa ndefu
 
Lwanga in
Morrrison Out.

Mudi amchukue mmojawapo Kati ya Hawa.
Aziz Ki,Adebayo wa USGN(Japo Ni mbahili na kuwang'oa hao nyota Ni shughuli).Tunahitaji mchezaji wa kuanza kwny mechi na si aina ya kina Morison,Benchi sana pesa ndefu
Si rahis kuwapata hao. pia watu hawafaham madhara ya propaganda anazofanya boss wetu Mo kuwa Simba ni tajir Africa.

Tukiwagusa kina Aziz Ki tutaambiwa Ada isiyopungua billion.
 
Siku chache kabla ya pambano la ugenini dhidi ya Asec Mimosas ,, boss mkubwa wa Simba Try Again anasikika akitamba kwamba Simba itasajili Wachezaji wanne wa kigeni mwishoni mwa msimu. Kipigo dhidi ya Asec kilianzia hapo....
Ufalme wa Simba umefitinika, mnagombana wenyewe kwa wenyewe.

Wawa ni 51 yrs sasa, Onyango 52, Kagere 48. Mnategemea nini?

Hiyo sio timu ya mpira ila ni timu ya makumbusho ya vipaji vya mpira
 
Kwa akili zako unadhani simba hii sawa na ile iliyocheza club bigwa miaka ya nyuma? Halafu nyie nyie ndio mnatakaa matokeo mazuri? Sema nyie mashabiki wa simba akili zenu mnazijua wenyewe watu wa low capacity thinking
ile si ilikuwa inapulizia sumu vyumbani au?
 
Wewe ni kibwengo cha Manara
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…