Tetesi: Salim Abdallah ‘Try Again’ katika jaribio la kumng’oa Mo Dewj Simba!

Uzi bado unadunda ama sasa ndiyo umefikia kikomo?

Hebu tuambie madam, isijekuwa vita sasa inahamia nje.
 
Uzi bado unadunda ama sasa ndiyo umefikia kikomo?

Hebu tuambie madam, isijekuwa vita sasa inahamia nje.
Tunamsubiria tajiri mwenye masimango atoe tangazo kwa umma!

Ndani ya dk 35 kutoka sasa taarifa atakuwa ameitoa
 
Mo arejea kama Mwenyekiti wa bodi na kamteua Try Again kua mjumbe wa Bodi, kiko wapi sasa?

Tuliwambia mapema hizi taarifa ni feki zipuuzeni mkakaza shingo, mkamwaga misifa kwa mzushi uchwara, akawa anatupiga vijembe

Mzushi uchwara katelekeza uzi kwa aibu ya kuaminisha watu uongo, na walioukubali uongo wa mzushi uchwara wanaupita uzi kama vile wanaaga maiti iliyopata ajali ya moto
 
Unaongelea hasira, wazee wa kusambaza taarifa za uongo mmepanic baada ya mambo kwenda tofauti na uzushi wenu,

Mo karudi kama mwenyekiti wa bodi na try again kateuliwa kua mjumbe, hii ni ngumi ya mdomo kwenu nyinyi wazushi wote sasa mmepagawa, jishikilieni ufalme wa mnyama unarejea, ile miaka 4 ya umwenyekiti wake mlipitia mateso makali sana lazima muogope mtetemeke

Simba ipo Imara mashabiki na wanachama tunamkubali Mo na tunamuamini, nyinyi mnaumia nini?

"Mo,Ninarejea nikiwa na nguvu na ari mpya mpaka Simba itakaporejea kwenye hali yake ya kawaida", amesema Dewji na kuongeza:-

"...naongozwa zaidi na ushabiki wa Simba, siyo uwekezaji, wala ufadhili wala udhamini......sitaiacha Simba leo wala kesho".
 
Reactions: Tsh
Watu wa kuzusha na kusambaza taarifa za uongo
Mimi nashangaa mnapoteza muda kusikiliza uzushi.Si huyo huyo aliyedai eti Hersi anatoka na Mobeto.Eti mdhamini ni shemeji yake yaani GSM.Wakati Hersi ameoa Arusha wala hajaoa dada wa mdhamini wa Yanga.Ni mzushi njaa apuuzwe.
 
Sasa tusubiri usajili.
 
Huyu dada ni muongo sana
 
Huyu dada ni muongo sana
Hivi wewe una akili timamu kweli? Habari niliyoileta ilikuwa vita ya madaraka kati ya Mo na Salim, na niliuliza kabisa ni nani ataibuka mshindi?

Sikuweka hitimisho la kwamba Mo atashindwa, na ni kweli kwamba vita ilikuwepo baina yao na wengi waliripoti.

Uongo uko wapi?
 
Unavuthibitisho wa hiyo vita uuweka hapa? Yani watu wawe kwenye vita ya madaraka wateuane tena inakuingia akilini.?

Kwenye conent ulikua unatamba na kuzodoa watu kwa kujifanya taarifa yako ni ya kweli.

Chutama dada umepuyanga, tulikuambia toka mwanzo kua huu ni uzushi ukashupaza shingo

Ukaja na Uzi mwingine wa kuhusu Eng Hersi na mke wake eti ni shemeji yake GSM, kitu ambacho si kweli

Punguza uongo na uzushi
 
Reactions: Tui
Halafu wanamuita eti jasusi.,[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
Jasusi my kimba! [emoji706]
 
Sikia, sijakulazimisha kusoma ninavyoandika. Kama unaona ni uzushi si uache kufuatilia? Uzushi na bado unasoma kila ninachokileta?

Acha kufuatilia taarifa/habari ninazozileta, simple.
 
Halafu wanamuita eti jasusi.,[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
Jasusi my kimba! [emoji706]
Halafu kila uzi ninaouleta mmejaa tele 😂😂
 
Sikia, sijakulazimisha kusoma ninavyoandika. Kama unaona ni uzushi si uache kufuatilia? Uzushi na bado unasoma kila ninachokileta?

Acha kufuatilia taarifa/habari ninazozileta, simple.
Siwezi Kuacha Kusoma Nyuzi humu Jf, na Siwezi kuukalia kimya uongo na Uzushi,

Jasusi wa Mchongo
 
Reactions: Tui
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…