Salim Almas CUP 2023 Mshindi wa Kwanza Aondoka na Kitita cha Milioni 26

Salim Almas CUP 2023 Mshindi wa Kwanza Aondoka na Kitita cha Milioni 26

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2020
Posts
2,833
Reaction score
1,301

SALIM ALMAS CUP 2023 MSHINDI WA KWANZA AONDOKA NA KITITA CHA MILIONI 26

Mbunge wa Jimbo la Mahenge/Ulanga Mhe. Salim Alaudin Hasham ametoa Shilingi Milioni 26 katika siku ya Fainali za Michuano ya Salim Almas CUP iliyochezwa katika Viwanja vya Shule ya Msingi Mwaya ili kuunga mkono maendeleo ya jimbo.

Mgeni rasmi katika Fainali za Salim Almas CUP 2023 alikuwa ni Naibu Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Hamis Mwinjuma (MwanaFA) zilizofanyika mnamo tarehe 28 Oktoba, 2023 kwa lengo la kukuza Vipaji na Burudani kwa Vijana na wapenzi wa Michezo katika Jimbo la Ulanga Mkoani Morogoro.

Naibu Waziri, Mhe. Hamis Mwinjuma amempongeza Sana Mbunge wa Jimbo la Ulanga kwa kuendelea kutekeleza Ilani ya Chama Cha Mapinduzi kwa kuendelea kuunga Mkono Shughuli za Maendeleo Jimboni.

Aidha, Mbunge wa Jimbo la Ulanga, Mhe. Salim Almas Alaudin ametoa Shilingi Milioni Nane na laki Nne (Tsh.8,400,000/) kwaajili ya kujengea vivuko maeneo ambayo Wananchi wameomba kujengewa

VileVile, Mhe. Salim Almas Alaudin ameahidi kutoa Shilingi Milioni 26 kwa mshindi wa kwanza wa mashindano na kusema ili kuchochea maendeleo ya wananchi wa Ulanga na Kuunga Mkono Jitihada za Serikali inayoongozwa na Rais Dkt Samia Suluhu Hassan katika Elimu, zawadi ya Milioni 26: Milioni moja itakuwa ya Timu (1,000,000/) na Milioni Ishirini na tano Itajenga Darasa kuunga Mkono maendeleo.

Pia, Mbunge ameahidi kuanzia tarehe 15/11/2023 ataanza ziara yake ya Kutembelea Wananchi wa Jimbo la Ulanga kwa kila Kata ili kusikiliza kero zao na kutatua zile ambazo zipo ndani ya uwezo wake

🇹🇿🇹🇿🇹🇿🙏🙏🙏

#KaziIendelee

WhatsApp Image 2023-10-29 at 14.20.24.jpeg
WhatsApp Image 2023-10-29 at 14.20.39.jpeg
WhatsApp Image 2023-10-29 at 14.21.02.jpeg
WhatsApp Image 2023-10-29 at 14.20.58.jpeg
WhatsApp Image 2023-10-29 at 14.20.30.jpeg
WhatsApp Image 2023-10-29 at 14.21.09.jpeg
 

SALIM ALMAS CUP 2023 MSHINDI WA KWANZA AONDOKA NA KITITA CHA MILIONI 26

Mbunge wa Jimbo la Mahenge/Ulanga Mhe. Salim Alaudin Hasham ametoa Shilingi Milioni 26 katika siku ya Fainali za Michuano ya Salim Almas CUP iliyochezwa katika Viwanja vya Shule ya Msingi Mwaya ili kuunga mkono maendeleo ya

Pia, Mbunge ameahidi kuanzia tarehe 15/11/2023 ataanza ziara yake ya Kutembelea Wananchi wa Jimbo la Ulanga kwa kila Kata ili kusikiliza kero zao na kutatua zile ambazo zipo ndani ya uwezo wake

🇹🇿🇹🇿🇹🇿🙏🙏🙏

#KaziIendelee
Uchaguzi umekaribia hukuna maendeleo mliyoyafanya mnawahadaa wananchi na mabonanza uchwara
 
Huu usanii sasa. Sasa hapo inakuwaje zawadi ya Mil. 26 kwa timu ikiwa Mil. 25 inaenda kwenye ujenzi.

CCM kila kitu kwao ni magumashi.
 
Ayo makombe ya kienyeji ndio ya jamii ya Abiola cup ambalo Simba alifika fainal mwaka 1993.
Mshindi anapewa medali za sido na ubwabwa na anayepoteza anapewa sahani ya ubwabwa maharagwe.
 
Back
Top Bottom