Stephano Mgendanyi
JF-Expert Member
- May 16, 2020
- 2,833
- 1,301
SALIM ALMAS CUP 2023 MSHINDI WA KWANZA AONDOKA NA KITITA CHA MILIONI 26
Mbunge wa Jimbo la Mahenge/Ulanga Mhe. Salim Alaudin Hasham ametoa Shilingi Milioni 26 katika siku ya Fainali za Michuano ya Salim Almas CUP iliyochezwa katika Viwanja vya Shule ya Msingi Mwaya ili kuunga mkono maendeleo ya jimbo.
Mgeni rasmi katika Fainali za Salim Almas CUP 2023 alikuwa ni Naibu Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Hamis Mwinjuma (MwanaFA) zilizofanyika mnamo tarehe 28 Oktoba, 2023 kwa lengo la kukuza Vipaji na Burudani kwa Vijana na wapenzi wa Michezo katika Jimbo la Ulanga Mkoani Morogoro.
Naibu Waziri, Mhe. Hamis Mwinjuma amempongeza Sana Mbunge wa Jimbo la Ulanga kwa kuendelea kutekeleza Ilani ya Chama Cha Mapinduzi kwa kuendelea kuunga Mkono Shughuli za Maendeleo Jimboni.
Aidha, Mbunge wa Jimbo la Ulanga, Mhe. Salim Almas Alaudin ametoa Shilingi Milioni Nane na laki Nne (Tsh.8,400,000/) kwaajili ya kujengea vivuko maeneo ambayo Wananchi wameomba kujengewa
VileVile, Mhe. Salim Almas Alaudin ameahidi kutoa Shilingi Milioni 26 kwa mshindi wa kwanza wa mashindano na kusema ili kuchochea maendeleo ya wananchi wa Ulanga na Kuunga Mkono Jitihada za Serikali inayoongozwa na Rais Dkt Samia Suluhu Hassan katika Elimu, zawadi ya Milioni 26: Milioni moja itakuwa ya Timu (1,000,000/) na Milioni Ishirini na tano Itajenga Darasa kuunga Mkono maendeleo.
Pia, Mbunge ameahidi kuanzia tarehe 15/11/2023 ataanza ziara yake ya Kutembelea Wananchi wa Jimbo la Ulanga kwa kila Kata ili kusikiliza kero zao na kutatua zile ambazo zipo ndani ya uwezo wake
🇹🇿🇹🇿🇹🇿🙏🙏🙏
#KaziIendelee