Atukuzwaye
Senior Member
- Oct 5, 2026
- 191
- 250
Naibu Mkurugenzi Mkuu wa Crown Media, Salim Kikeke amesema Afrika ina uwezo wa kufanya maamuzi kuhusu masuala yake yenyewe na kuchagua washirika wa kufanya nao kazi bila kutegemea mataifa mengine.
Kikeke amesema hayo katika mahojiano na kituo cha habari cha RT jijini Moscow, Urusi, alipokuwa akishiriki Mkutano wa Afrika na Urusi. Amesema kumekuwa na majukwaa mbalimbali ya ushirikiano yanayohusisha Afrika na mataifa mengine, ikiwemo Marekani, Italia na Urusi, akieleza kuwa bara hilo lina nafasi ya kuamua aina ya ushirikiano unaolinufaisha.
Ameongeza kuwa Afrika inapaswa kutumia fursa zilizopo kuimarisha uwezo wake wa kufanya maamuzi na kushiriki katika ushirikiano wa kimataifa kwa kuzingatia maslahi yake.
Soma pia: Kumbukizi: Mkutano wa Berlin ulioamua mustakabali wa Afrika bila Waafrika kushirikishwa