Salim Kikeke wa BBC ateuliwa kuwa balozi wa Simba SC nchini Uingereza

johnthebaptist

JF-Expert Member
Joined
May 27, 2014
Posts
97,869
Reaction score
171,716
Mtangazaji mahiri wa Shirika la Utangazaji la Uingereza BBC mh Salim Kikeke ameteuliwa kuwa balozi wa Simba SC nchini Uingereza.

Klabu ya Simba imesema inategemea Kikeke atawapaisha sana kimataifa ikiwemo kuwasajilia wachezaji kutoka ligi kuu ya nchi hiyo yaani Premier League.

Chanzo: Dira tv!
 
Hiyo kutaja tu kwamba kateuliwa kuwa balozi bila kumalizia kuwa kateuliwa kuwa balozi wa nini kwenye kichwa cha habari umeleta taharuki miongoni mwa jamii. Inatakiwa TCRA wakuchukulie hatua kama walivyofanya kwa Kwanza TV.
 
Source Dira tv!
haahaa huu utani sasa yani mikia isajili mchezaji kutoka EPL?
 
Mtangazaji mahiri wa Shirika la Utangazaji la Uingereza BBC mh Salim Kikeke ameteuliwa kuwa balozi wa Simba SC nchini Uingereza.

Klabu ya Simba imesema inategemea Kikeke atawapaisha sana kimataifa ikiwemo kuwasajilia wachezaji kutoka ligi kuu ya nchi hiyo yaani Premier League.

Source Dira tv!
Atusaide tumsajili Mane na Firmino ili tujihakikishie ubingwa wa VPL mwaka huu
 
Hiyo kutaja tu kwamba kateuliwa kuwa balozi bila kumalizia kuwa kateuliwa kuwa balozi wa nini kwenye kichwa cha habari umeleta taharuki miongoni mwa jamii. Inatakiwa TCRA wakuchukulie hatua kama walivyofanya kwa Kwanza TV.
Kwani kuwa balozi kunaleta taharuki gani?

Kwa mfano le mutuz Haji Manara Ali Kiba. Steve Mengere aka Nyerere wote hawa ni mabalozi mbona hakuna taharuki yoyote!
 
Mtangazaji mahiri wa Shirika la Utangazaji la Uingereza BBC mh Salim Kikeke ameteuliwa kuwa balozi wa Simba SC nchini Uingereza.

Klabu ya Simba imesema inategemea Kikeke atawapaisha sana kimataifa ikiwemo kuwasajilia wachezaji kutoka ligi kuu ya nchi hiyo yaani Premier League.

Source Dira tv!
Mimi nilijua jiwe kampa shavu ili aache kukoleza moto kule BBC kuhusu shangazi mwanasheria
 
Hii habari ni ya kweli, imewekwa Kwenye account za Simba toka jana. Ila swala kua awasajili wachezaji wa EPL ilo limeongezwa.
 
Bodi ya Wakurugenzi ya mabingwa watetezi wa ligi kuu soka Tanzania Bara Simba SC imemteua Mtangazaji mashuhuri wa shirika la Utangazaji la Uingereza (BBC), Salim Kikeke kuwa Balozi wa Simba Sports Club nchini London.

Kupitia ukurasa wa Twitter Mohammed Dewji ameandika “Bodi ya Wakurugenzi tumemteua Mtangazaji wa BBC, Ndg. Salim Kikeke kuwa Balozi wa Simba Sports Club wa mji wa London, Uingereza. Hongera Salim Kikeke, tunaimani na wewe utaipeperusha vyema bendera ya Simba”.
@ Millard Ayo
 
Mtangazaji mahiri wa Shirika la Utangazaji la Uingereza BBC mh Salim Kikeke ameteuliwa kuwa balozi wa Simba SC nchini Uingereza.

Klabu ya Simba imesema inategemea Kikeke atawapaisha sana kimataifa ikiwemo kuwasajilia wachezaji kutoka ligi kuu ya nchi hiyo yaani Premier League.

Source Dira tv!
Kwa hiyo awasalijilie Simba wachezaji kutoka EPL ili waje kucheza VPL kweli ?
 
Mo anacheza na akili za mikia tu,angalia wanavyotumia nguvu nyingi kuhakikisha Yanga aifikii walipofika wao msimu uliopita huku wakiwa hawana mtu kama mo,Yanga inasuffer kwa sbb manji alihaminisha Yanga haiwezi kufanikiwa chochote bila yeye,na ndivyo mo alivyowaaminisha mikia,wahindi sio watu wazuri kabisa
 
Back
Top Bottom