Raia tuna haki na dhima ya kukumbushana wajibu wetu wa kulipa kodi....
Inawezekanaje tukauendesha uchumi tuutakao kwa WALIPA KODI MILIONI 3 kati ya sisi raia milioni 62?!!!
Tunataka nchi itufanyie....imeshatufanyia sana mathalani AMANI NA UTULIVU TULIONAO tukiendelea kubangaizia shughuli zetu bila bugdha kama Somalia ,Burundi ,Rwanda na Sudan....
Swali....
Je tumeifanyia nini NCHI YETU ?!!
Je tunaifanyia nini NCHI YETU ?!!
Hapa ndipo ilipo MIILI YETU tukiwa hai ,na makaburi yetu tukizikwa na MIZIMU YETU baadaye haitozungukia Uganda ,Kenya wala Malawi bali nyumbani Tanzania[emoji7]
#Tutafakari