GE2025 Salim Morcase: Palipo na vurugu hakuna shughuli za kiuchumi zitafanyika

GE2025 Salim Morcase: Palipo na vurugu hakuna shughuli za kiuchumi zitafanyika

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025

DuaZaMama

JF-Expert Member
Joined
Jun 2, 2025
Posts
1,882
Reaction score
4,153
Kuelekea Uchaguzi Mkuu wa Rais, Wabunge na Madiwani wananchi wamehimizwa kutunza na kulinda amani katika maeneo yao ili waendelee kufanya shughuli zao za kiuchumi kwa utulivu na usalama. Hayo yamesemwa Oktoba 23, 2025 na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Pwani, Kamishna Msaidizi wa Polisi, Salim Morcase alipokua akizungumza na wanachi katika kipindi cha Amka na Chalinze cha Chalinze FM 97.5 ambapo aliwaeleza wananchi wajibu wao na umuhimu wa kutunza amani ya nchi.

Kamanda Morcase alieleza kuwa pasipo na amani hakuna shughuli za kiuchumi zitakazofanyika kwani kila mmoja atakua anahangaika huku na kule kuinusuru nafsi yake isipate madhara hivyo kukosa uhuru wa kufanya shughuli hizo. Akisisitiza utii wa sheria za nchi Kamanda Morcase alieleza kuwa kabla mwananchi hajakubali kushawishiwa kushiriki kwenye kitendo chochote ni lazima ajiulize kama sheria zinamruhusu kufanya hiivyo ili kama hazimruhusu ajiepushe na kitendo hicho ili kujilinda yeye na kulinda amani ya nchi.
 
Haki iko wapi?
Huyo AMANI mme wake HAKI
Kwanini wanamfunga mikono?
 
Back
Top Bottom