Sallam athibitisha Harmonize kujiondoa WCB

Sallam athibitisha Harmonize kujiondoa WCB

Ndugu kama hujui mambo bora ukakaa kimya na huyo harmonize mnaempa kichwa nyie mtakuja kuanza kumuonea huruma wenywe kwa vile hujui ngoja nikwambie kwan WCB Mondi mwenywe akifanya shoo 30% ya pesa aliyoingiza inaenda kwa hao mameneja wa tatu yaani mshahara maana ndo makubaliano yeye harmonize ni nani mpaka asitoe hiyo 30% kwa mameneja na pesa kidogo kwenye mfuko wa lebel kwa Mondi kurudisha pesa zke.

Af watu hamjui uzito wa LEBEL mfano KANYE WEST na mipesa yake yote ile lakini yupo chini ya Jay Z na halalamiki na anakatwa asilimia flani kama kawaida.
Na lebel cku zote huwa zinamashabiki wake mfano tu kwa maono yangu lavalava sio msanii kiviile na nyimbo zake Mara nyingi huwa hazieleweki lakin lakini akitoa ngoma kaa kama siku nne hivi af ingia YouTube uone alivyopata viewers wengi na ndo mashabiki hao wa WCB ndo wanao mpa support wakati huohuo rich mavoko anatoa ngoma kupata 500k ni kwa tabu sana kwa hiyo nachotaka kusema kuwa lebo ina mashabiki wake harmo akiondoka WCB asilimia kubwa atajitenga nao na kuwa maadui wake

Wewe ni kati ya wasioujua muziki lakini una ujuaji mwingi ilhali huna ulijualo.
Unasema Lavalava sio msanii na nyimbo zake hazieleweki? Mimi sio shabiki wa hiyo WCB yenu ila Lavalava ndio msanii wangu bora pale WCB na hizo nyimbo zake unazosema huzielewi ndio nimejua hujui muziki.

Unathubutuje kusema mtu mwenye vibao vitamu kama Bora Tuachane, Utatulia, Go Gaga na wimbo wangu bora wa muda wote kwa Lavalava, Kilio sio msanii?
Wewe jamaa umejua kuniharibia asubuhi yangu!
 
Wabongo ni wanafiki tu.

Kipindi kile wasanii wakiachana na CMG au THT tunaambiwa wamejitambua na blah blah kibao ila huyo jamaa kutoka WCB imekuwa nongwa Why?
Mkuu humu JF member wengi wanashabikia wcb so yeyote akitoka pale atanangwa balaa, lkn mtu akitoka CMG wanashangilia.
Uchawi, roho mbaya na unafiki humu ndio mahali pake!
 
No offense, ila asilimia kubwa ya vijana wa kusini kwa kweli si watu wakusema unaweza ukawa na ushikaji nae ili mfanikishe jambo na likatiki mazima, tena hususani wale waliolelewa kulekule, achana na hawa waliozaliwa ocean road, nazungumzia wale wa shule ya msingi kulekule.
Wapo hivi, asilimia kubwa kwanza wanatoka kwenye familia duni na wajinga, sasa akikuona wewe mambo yako supa huwa wanajipendekeza kwako sana, anaweza mtoto wa kiume akaja hadi kwako mwanaume mwenzake kukufulia, kupiga deki, kukupikia ili mradi umuone msela safi. Mnapanga mipango mfanyeje ili mpate kipato cha ziada kupitia yeye kwakuwa kipindi hicho hana mchongo wowote wa maana, unaona sio kesi, ngoja nitoe milioni zangu tufungue duka, au umnunulie bodaboda, au hiace yeye asimamie, au umwendeleze kipaji chake n.k kiroho safi.
Akisha ijua biashara fresh, anaanza kukuvimbia, anajiona bila ya yeye wewe hulambi kitu, anakuona kama ile hela mliyokubaliana akupatie kwa siku au wiki ni kama anakupa bure, anasahau pesa ya uwekezaji yote hajatoa hata senti, yeye ni nguvu kazi tu. Wakikutana na wenzake wanajazana ujinga mwishoe anakukimbia, na huwa hawachukui round wanafeli vibaya mno.
Hili la harmonize halijanishtua kwa vyovyote, ni kitu nilitegemea, nilipoona mazingira ya kwao akituonyesha nikajua huyu, diamond kalamba galasa hapa, ajitahidi diamond arudishe hela yake ya uwekezaji, amuache aende.
Kuna watu watasema dogo amekua sasa ni muda wa yeye kujitegemea, mnazidi kumjaza ujinga. Muda utaongea. Hivi mnadhani kuwa na lebo yenye studio, radio na tv ni kitu simple eeeh kama kuwasha kwa remote?
 
Mkuu achana nae huyo, hawa ndo huwa wanaamini mchezaji ni mkubwa kuliko team... Watu wanaoangalia final product (music) wanaweza kuona kama Harmonize ni mkubwa, ila kiuhalisia bila management ya wcb huyo Harmonize angeendelea kuuza mitumba tandale hadi leo.. Harmonize kakosea sana kubadili management, Kina Sallam hawana issue nyingine kubwa za kuwaingizia kipato zaidi ya kusimamia wasanii wao, wanaspend time yao 100% kwenye music wa wasanii wao, ila hiyo management ya sasa ya Harmonize ni watu ambao tayari wana channel zao za pesa, watakua na muda kidogo wa kusimamia msanii wao, na hapo ndo Harmonize atakapoanza kupotea.. Harmonize Hawezi kuwaingizia pesa zaidi ya wanazoingiza sasa kwenye Miradi yao.

Harmonize ni lini aliuza mitumba Tandale? Hii ni fact ndogo ambayo inaondoa maana ya yote uliyoyaandika.

Nawashangaa sana mnaosema Harmonize kakosea kubadili management... Hivi nyie mnaijua WCB kuliko Harmonize?
Harmonize ni mtu wa ndani wa WCB, anajua mengi kuliko mtu yeyote nje ya WCB. Acheni kuleta siasa ktk masuala ya career za watu.
Huu uchambuzi wenu hauna maana yoyote maana tasnia ya muziki inahusisha mambo ya ndani ambayo hatuyajui tofauti na mpira unaochezwa hadharani ndio maana mtu unaweza kufanya uchambuzi ila sio muziki wetu uliobeba fitna za kila namna.

Mimi naona tumtakie heri kijana wetu, ameonesha uthubutu muacheni asonge mbele acheni hizi ramli zenu chonganishi.
 
Kuna Dogo mmoja diamond alimchukua kutoka Sweden ndio kachukua nafasi ya Moses iyoyo kama dancer instructor Wa wcb, nimekutana nae face to face na anajuta kuingia wcb ... Huyo Dogo ndio kabuni dance styles kwenye nyimbo zote za wcb kuanzia mwaka Jana . nyegezi, tetema, inama n.k ...
Hizo style zinazochezwa kwenye hizo videos ulizotaja mbona video kibao za Nigeria wanazitumia kabla hata ya mwaka jana. Diamond kazichukua tu kazi-compile... Huyo unayesema kazivumbua mwambie akuambiye tena.
 
Harmonize ni lini aliuza mitumba Tandale? Hii ni fact ndogo ambayo inaondoa maana ya yote uliyoyaandika.

Nawashangaa sana mnaosema Harmonize kakosea kubadili management... Hivi nyie mnaijua WCB kuliko Harmonize?
Harmonize ni mtu wa ndani wa WCB, anajua mengi kuliko mtu yeyote nje ya WCB. Acheni kuleta siasa ktk masuala career za watu.
Huu uchambuzi wenu hauna maana yoyote maana tasnia ya muziki inahusisha mambo ya ndani ambayo hatuyajui tofauti na mpira unaochezwa hadharani ndio maana mtu unaweza kufanya uchambuzi ila sio muziki wetu uliobeba fitna za kila namna.

Mimi naona tumtakie heri kijana wetu, ameonesha uthubutu muacheni asonge mbele acheni hizi ramli zenu chonganishi.
Utter truth & facts. Nuff said, Miss.
 
Hatimaye meneja wa WCB Sallam SK amekata mzizi wa fitna baada kuthibitisha Harmonize kaandika barua ya kuvunja mkataba na lebo ya WCB Wasafi.

Amesema kwa sasa wanasubiria kufanya taratibu za kisheria kuuvunja mkataba na soon watakuwa na kikao cha kukubaliana terms ingawa Harmonize ameshaonyesha nia ya kukubaliana na terms zote za kuterminate mkataba.

Sallam ameomba radhi kwa mwenendo uliokuwa unaonyeshwa na msanii huyo siku za karibuni lakini amewaomba mashabiki wa Wasafi waendelee kutoa sapoti kwa Harmonize kwani ajaondoka kwa ubaya.

Mtazamo wangu; Harmonize anaenda kuwa historia kwenye muziki wa bongofleva uenda tukashangaa sana pale ambapo hatutasikia tena muziki wa kueleweka kutoka kwake na ukawa mwisho wake kisanaa.

Waliomshauri Hamo anapaswa kuwachukia maisha yake yote kama waliomshauri Mavoko.
Usikariri maisha wewe
 
Atakamata soko la Lindi, Mtwara, Masasi mpaka Nachingwea yote. Nangumene wote lazima wampe support wa nyumbani.
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Dua la kuku........... kwani mtu akikua c anaondoka kwa wazazi wake mbona mmemuwekea kinyongo au lebo ndo inamtegemea yeye akiondoka kuna mkwaja utakata???
We jamaa siku zote umekazana mtoto akikua anaondoka kwa wazazi. Mavoco mlisema hivyo hivyo,yuko wapi?. Kumbuka hao waliomshauri kuondoka wanamtegea sana kuchuma kutoka kwake,hawana ujanja wa kuupush mziki wake zaidi ya kuchuma. Umoja ni nguvu,huko alikoondoka ni team
 
Time will tell atarudi kuwalaumu Wasafi ndio wanamkwamisha.. Hamo hana talent ya kusimama nje ya Wasafi evidence project yake na Q chilla imeangukia pua pamoja na mkwanja mrefu alioweka
Kabisa mkuu. Muda si muda atarudi kulia wasafi wanamkwamisha.
 
Time will tell atarudi kuwalaumu Wasafi ndio wanamkwamisha.. Hamo hana talent ya kusimama nje ya Wasafi evidence project yake na Q chilla imeangukia pua pamoja na mkwanja mrefu alioweka
Katika maisha hivyo ni vitu vya kawaida sana.
Is it better to try and fail than not try at all,Life is about trial, error and Imrovement.
 
Label ziko nyingi mimi nlijua labda amesign label ya nje ambayo ingembeba zaidi ya wcb.tuwe wakweli jembe hawezi kumjenga kumziki mana hajawahi kumsimamia msanii yeyote kimuziki,yetu macho na masikio tutaona yajayo
pale wasafi kuna watatu au unaweza kuuita utatu mtakatifu, ambao ni sallam, babu tale na saidi fella.

ukiondoa ushirikina wao, fitna na propaganda zao ambazo kwa mda mrefu wamekuwa wakizitumia ku monopolize music industry ya tanzania, kazi nyingine kubwa pale wasafi ni kujineemesha kwa kupitia wasanii walio chini ya lebel ya wasafi.

unakuta kwa mfano malipo ya show moja ya rayvanny, hao wote watatu kila mtu ana parcent yake na hajaitolea jasho. nampongeza sana harmonize kwa kuachana na hao wapuuzi watatu. na ninamsifu kwa ku sign chini ya jembe jembe.

najua sallam na hao wapuuzi wenzie hawatakubali kushindwa kirahisi, lazima watajiribu kutaka kumvurigia deal lake la harmonize ila hawataweza maana jamaa pia ni born town, ana connection kubwa na pesa ya kula anayo.

hawa wapuuzi watatu kiboko yao alikuwa ni marehemu ruge mutahaba the master minder. rest in peace ruge.
 
Wewe ni kati ya wasioujua muziki lakini una ujuaji mwingi ilhali huna ulijualo.
Unasema Lavalava sio msanii na nyimbo zake hazieleweki? Mimi sio shabiki wa hiyo WCB yenu ila Lavalava ndio msanii wangu bora pale WCB na hizo nyimbo zake unazosema huzielewi ndio nimejua hujui muziki.

Unathubutuje kusema mtu mwenye vibao vitamu kama Bora Tuachane, Utatulia, Go Gaga na wimbo wangu bora wa muda wote kwa Lavalava, Kilio sio msanii?
Wewe jamaa umejua kuniharibia asubuhi yangu!
Umehadimika.
 
Mkuu acha kabisa kuna siku huyo rayvan kakosa hela ya mafuta kutoka kwake tabata mpaka Mbezi .. Wengi Wa mashabiki wanadanganywa na zile picha za Instagram tu ...


Watu hawawezi amini kuwa rich mavoko licha ya kutoa zile hitsong alikuwa hana hata mia mfukoni na akipata show hao utatu mtakatifu wanachukua cha kwao na Wcb kwa ujumla na kinachobaki ndio anapewa...


Kuna Dogo mmoja diamond alimchukua kutoka Sweden ndio kachukua nafasi ya Moses iyoyo kama dancer instructor Wa wcb, nimekutana nae face to face na anajuta kuingia wcb ... Huyo Dogo ndio kabuni dance styles kwenye nyimbo zote za wcb kuanzia mwaka Jana . nyegezi, tetema, inama n.k ...
Rayvan huyu huyu ambae baby mama wake alituambia wanatumia mil. 9 kwa photoshoot?
 
Katika kitu Harmonize amefanya kikubwa katika maisha yake ni kuingia WCB na kizuri kikubwa zaidi nI kutoka WCB naamin ameshapata platform ya mashabiki wa kutosha ni vema sasa aishi maisha yake sio kusindikiza tena kuna mtu hapo amesema kwamba kama4 Diamond anakatwa 30% ya show inaingia kwa hao mameneja yeye ni nani asikatwe hiyo % lakin mimi naona huo ni ujinga mkubwa sana yaani manager watatu wachukue 30% bado manager wake nae achukue bado nyingine ibaki kwa kampuni cmon! Labda kama show inalipa 100m but hamna show ya namna hiyo na kijana hapo ndio akaanze kufanya maisha sasa ya uhalisia wala asikatishwe tamaa na hawa washabiki wa WCB maana kama Jux anaishi hayupo wcb, Aslay anaishi maisha mazuri tu yeye kwa nini ang'ang'ane na maisha ya kishowoff platform aliyonayo inamtosha kutoboa kimaisha ukipata chochote sasa ni cha kwake hakuna kugawana sijui na manager watatu wala wcb namuonea huruma tu Rayvan bado hajapata akili ya maisha ila kama akifumbuliwa macho ndio ataelewa ila abaki kwanza atengeneze jina na akili ipanuke
 
Tungoje kwanza kabla ya kutoa neno la kulaumu. Kwanza walinzi wake. Pili zihara za USA. 9Ja. Tatu kampeni za CCM zitampandisha nk ...
 
Back
Top Bottom