Sallam SK aelezea baada ya kupona ugonjwa wa Corona

Sallam SK aelezea baada ya kupona ugonjwa wa Corona

Hziyech22

JF-Expert Member
Joined
Jun 8, 2019
Posts
15,351
Reaction score
21,362
Manager wa msanii mkubwa Diamond Platnumz, Sallam SK amefunguka baada ya kupona ugonjwa wa Corona akiwa amefanyiwa na moja ya chombo cha habari amesema kwamba wakati anatangaza kuwa amepata Corona ndugu zake wa karibu, waliudhunika na wengine kuanza vilio pamoja na wadau mbalimbali wa mziki na sector nyingine na wakajua muda si mrefu nitakufa.

Na inatokea hivi kwasababu media nyingi zinatoa habari mbaya za ugonjwa huu za vifo na wagonjwa wakati kuna wengine wengi tu wanapona hawazipi uzito mkubwa sometime unakuta mtu kafa kwa ugonjwa mwingine lakini kwa habari zao wanasema kafa kwa corona tuna tengeneza taaruki kubwa kwa watu kiasi ambacho wengine wanakosa amani.

Akaongeza zaidi kutoa ushauri kwa watu wajikinge kwa kufuata maelezo ya waatalamu wa Afya na Tasisi zinazotoa taarifa za ugonjwa Huu wasitengeneze taaruki kubwa kwa watu.
 
Back
Top Bottom