Eyce
JF-Expert Member
- Mar 16, 2016
- 7,185
- 24,330
Watu hamjui mziki ulianza kuharibika tokea arudi Ali Kiba kwenye game 2013,hapa ndipo zikaanza timu kwenye Kili Music Awards (Team Mange, Team Joketi, Team Wema na Team Kiba),mwisho wa siku tuzo chali.
Mistake kubwa tena kuliko zote media kuchagua upande kwenye hili beef la Kiba na Mondi, Matokeo yake sasa hivi tuna team Harmonize, mziki wabongo kila siku unazidi kivunjika, hatujui kesho tutakuwa na team ipi. Ukirudi kwa washika dau kila mtu na msanii wake, kila radio na wasanii wake, uadui unakua kila siku. Jana Joh na Sallam,leo Mb Dog na Ay kesho hatujui nani na nani.
Wanaija ni wabinafsi kila mshikadau kwenye Industry yao wanautizama mziki wao tu na wamesambaa sana kwenye vyombo vya kimataifa na hata ukifanya nyimbo na msanii wa Naija hawa upromoti hata kwenye acc zake za social networks,Shata Wale na Stoneboy waliya ongea haya.
Bongo sizani na wala sifikiri kama wasanii watapendana,kunawasanii wanaambiwa na media ukifanya collabo na msanii fulani hupati airtime, siku hizi washaanza kuitana wachawi (nishike mkono tushindane........) na fununu nilizo zipata sasa Country Wiz amesha jitoa Konde Gang, sijui napo itakuwaje kama watakuwa hawa jaachana vizuri.
Hizo team za udaku ni za kawaida na naweza kusema ni legacy ya mahaba ya watu kwa wema. Hizo team zari sijui diamond zilikuja lately japo Team kiba na Diamond zilidandia mbeleni na kweli zimekita mizizi on top kiasi kwamba wengine hawana chance
Pia muziki haukuharibikia kwa ali kiba kupewa promo ili awe replacement ya diamond kwenye industry maana hiyo michezo ya Watu wa "media flani" kupromote msanii flani ili ampoteze msanii mwingine ni kawaida. Hata lady jay dee alichezewa mbona, baada ya machozi band ikaundwa skylight band na ikapewa promo hadi machozi ikaanguka
Muulize rama dee au vumilia alipoleta kiburi. Muziki ulianza kuharibika ulipoanza kuwa commercial na watu wachache walio na koneksheni mjini kuamua nani aende na nani asiende. Sadly hata waliobaniwa washaujua utamu wa huu mchezo na wao wanaendeleza kwa hiyo hauishi leo wala kesho