Salma Kikwete: Jimbo langu la Mchinga halina Stendi hata moja

Richer

JF-Expert Member
Joined
Jun 9, 2025
Posts
2,318
Reaction score
4,079
Mbunge wa Mchinga Mkoani Lindi Salma Kikwete, kwenye kipindi cha maswali na majibu amehoji Serikali ina mpango gani na Jimbo lake halina Stendi hata moja wakati Magari makubwa yanapita kutoka Mikoa mbalimbali kama Ruvuma na Mtwara na mengine kutoka Nchini jirani ya Msumbiji.

Akijibu swali hilo, Naibu Waziri wa TAMISEMI Reuben Kwagilwa, amesema Serikali itafanya mapitio pamoja na kutathmini hali ilivyo ili kujenga stendi katika Jimbo hilo la Mchinga โ€œSerikali itafanya mapitio pamoja na kutathmini hali ilivyo Mchinga, ni muhimu sana Mji huo uwe na stendi hivyo sisi Serikali tutafanya mapitio na kuainisha cha kufanyaโ€


Your browser is not able to display this video.
 
Hasara kwa Taifa.
 
Watu wanataka mseme shida zao.
Safi sio mbaya kajenga hoja.
 
๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚๐Ÿšฎ๐Ÿšฎ๐Ÿšฎ๐Ÿšฎ๐Ÿšฎ๐Ÿšฎ๐Ÿ–•๐Ÿ–•๐Ÿ–•๐Ÿ–•๐Ÿ–•
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn moreโ€ฆ