Nilifuatilia kwa makini taarifa ile baada ya kusikia kuwa kanusurika na ajali. Alikuwa anafungua rasmi bweni la wasichana ambalo yeye na NGO yake ya WAMA amefadhili kulijenga na likaitwa kwa jina lakem baada ya mabinti wanafunzi katika Wilaya hiyo ya Serengeti kuathirika mno na mimba.
Taarifa aliyokuwa anapewa na Mkuu wa Mkoa ilihusu faida ya bweni hilo kwa wasichana kwa sababbu kwa mwaka jana pekee, wasichana zaidi ya 600 walipata ujauzito na hivyo kukatisha masomo yao kutokana na wao kupanga katika nyumba za wenyeji. Taarifa hiyo ilihusu shukrani zaidi na siyo taarifa ya maendeleo ya Mkoa. Hapa niko makini na sipendi upotoshaji. Mnyonge mnyongeni lakini haki yake mpeni.
Kuna wanao sema kuwa kuna harufu ya ka-ufisadi. Sasa mimi najiuliza, hivi mtu kufadhili mabinti zetu nayo imekuwa ufisadi ??? Kumbuka kuwa hata kule Rufiji nako kajenga shule ya wasichana kuwaokoa na tabia ya Wandengereko ya kuwaozesha wangali wadogo na wakiwa bado wanafunzi. Ubaya uko wapi jamani.?????
Bravo mama Salma Kikwete endelea na moyo huo huo, watu daima huangalia mabaya tu lakini mazuri hawayaoni wanakuwa na makengengeza.
Kuna mzushi mmoja kaja na hoja kwamba mama huyu anataka kugombea ubunge kwao Lindi, huo ni uongo wa mchana jamani. ACHENI UZUSHI HAPA JAMVINI.
Naona wewe hujui unachokiongea!! Maswali yetu ni haya;
1. Je mkuu wa mkoa alipaswa asome ile risala? Kwa nini isisomwe na mkuu wa shele ama mwenyekiti wa bodi ya shule? (iko wapi itifaki hapo kama si kujipendekeza?)
2. Anavyohutubia wananchi anahutubia kama nani na kwa minajiri ipi?
3. Je mke wa Rais ana mamlaka yoyote kikatiba hapa kwetu?
4. Je WAMA ni taasisi ya serikali? Kwa nini inatumia resources za serikali kama magari n.k.
5. Kwa nafasi yake kama mke wa Rais, je tutapimaje kama misaada inayotolewa kwa WAMA (based on her influence as the first lady) haitumiki kwa maslahi binafsi ya kwake na familia yake?
6. Kwa nini wakimaliza muda wao wa uongozi wanaondoka na taasisi zao?
7. Je huoni kwamba WAMA inatakiwa iwe responsible kwetu wananchi kwa sababu inatumia resources zetu kuanzia magari mpaka ofisi, sina uhakika na payroll, inawezekana pengine inatoka ikulu!!
Binafsi naona nchi hii inaendeshwa bila kufuata taratibu na best practice, mke wa rais ni mke kama walivyo wake zetu. Naamini anastahili ulinzi, mshahara na posho akisafiri basi. Haya mengine tunayoyaona ni mbwembwe tu za kikwere na yote yanatokana na watanzania kufubaa kiakili!
Vinginevyo tunatakiwa kuhoji haya mambo, kinyume na hapo siku Mama atakuja kumfukuza kazi waziri ama ofisa yoyote wa serikali kwa sababu naamini yeye na Mr. hawajui kama anavyofanya sasa si sahihi!! Wasaidizi wa rais pale ikulu wanajua haya si sahihi lakini hakuna mwenye ujasiri wa kumwambia Mama Salma wala Mkuu mwenyewe!