punainen-red
JF-Expert Member
- Nov 18, 2010
- 1,731
- 451
Hivi kuna siasa za chuki kuliko za mumewe! Wakati ule m-kwere anawazushia wenzake kina Salim huyu alikuwa mke wa nani? Kweli ukiwa mshirikina utamdhania kila mtu kuwa ni mshirikina! Siasa za chuki anazo m-kwere, ajabu huyu mama anajifanya haoni!'Siasa za chuki zinazoendeshwa...'
Mama gani asiye na huruma. Mimi najua wanawake ni watu wenye mioyo ya huruma naturally, sasa huyu asiyejua matatizo ya watz katoka wapi, nawashangaa hao waliokuwa wakimsikiliza na kumpigia makofi. Ndi hao wakipewa doti ya khanga wanapoteza network
mke wa rais wa jamhuri ya muungano wa tanzania salma kikwete, amesema ushindi wa kikwete katika uchaguzi mkuu wa mwaka jana hauna dosari kama baadhi ya vyama vya siasa vinavyotangaza.
Alitoa kauli hiyo mwishoni mwa wiki alipokuwa akizungumza na wanachama wa jumuiya hiyo mkoa wa dodoma kwa nia ya kuwashukuru kwa kazi kubwa waliyoifanya wakati wa kampeni ya uchaguzi mkuu mwaka jana.
mama salma alisema baadhi ya vyama vimekuwa vikitawanya maneno ya uwongo na kuulazimisha ulimwengu uamini kuwa walishinda katika uchaguzi mwaka jana.
"wanataka waiambie dunia kuwa wao ndio walioshinda, hivi walioshinda wana asilimia 20,"alihoji mama salma huku akishangiliwa na wanawake waliofurika kwenye ukumbi huo.
Alisema watu wanaoeneza uongo huo wanashangaza kwa kuwa tofauti ya kura kati ya ccm na vyama vingine ilikuwa kubwa sana.
Alibainisha kuwa uongo unaoenezwa na wapinzani umekuwa ukiwachochea wananchi kukichukia ccm wakati ukweli ni kuwa ccm ndiyo iliyoshinda uchaguzi huo.
alisema wengi wanaoshiriki katika uzushi huo ni watoto wao kwani wamebebwa na wao migongoni lakini sasa wanawazunguka kuwachafua.
"wasione simba kalowa wakafikiri ni paka akitoa makucha yake watakiona" alisema.
aliitaka jumuiya ya wanawake tanzania (uwt), kutokuwa wanyonge kukemea mambo yanayofanywa na baadhi ya vyama vya siasa dhidi ya chama cha mapinduzi(ccm).
Alisema uwt ni moja kati ya jumiya ya ccm hivyo ina haki ya kulaani kauli zinazotolewa na vyama hivyo.
"msiitegemee serikali peke yake kukemea haya hata nyie mnanafasi kubwa kwani serikali ni kila mtu,"alisema
alieleza kuwa siasa za chuki zinazoendeshwa na baadhi ya vyama vya siasa hapa nchini dhidi ya ccm ni tabia ambayo haipaswi kuachwa bila kukemewa.
Alifafanua kuwa ccm haiwezi kupoteza muda kulumbana bali itatumia muda huo kujadili mikakati yake iliyojiwekea katika mkutano mkuu uliofanyika mwaka jana.
Aidha, alisema ili jumuiya hiyo iweze kuendelea kuwa imara inahitaji kuwa na damu mpya ambayo ni vijana wasomi.
Alisema nia si kuwaoondoa wanachama ambao ni wakongwe bali ni kuweka mchanganyiko ambao utawezesha kuwepo na kasi mpya.
chanzo: Nipashe
Hapa ndo tunapopata wasiwasi, na ndipo uwezo wake finyu wa kufikiri unapojionesha wazi.... Ni bora angekaa kimya tu kuliko kuudhihirishia umma jinsi alivyo mbumbumbu!! Itawezekana vipi mtu ambaye alimchagua kwa kura yake leo aje kumchukia kwa kuambiwa tu, haiingii akilini kabisa!!
Mnategemea aseme nini zaidi ya aliyozungumza? Ni mropokaji mzuri tu huyu dada. Ebu muulize ana hakika ya anachokisema? hakika wengi watakutana na hukumu ya Mungu!