Nyendo
JF-Expert Member
- Jun 4, 2017
- 1,336
- 4,731
Mbunge Salome Makamba, amesema kuwa habari ya mabando kuisha muda wake baada ya kujiunga ni sawa na kuwaibia watanzania, adai kuwa ukijuinga bando la simu liwe la dakika za maongezi au la data unaweza usilitumie kutokana na changamoto nyingi sana zikiwemo za kukosekana kwa mtandao wa simu au mambo mengine, kulikata kisa muda kuisha si sahihi kwani kampuni za simu zinakuwa zimechukua pesa nyingi kwa watanzania ambayo walilipia ila hawajatumia huduma.
Amesema kuwa kampuni za simu zikichukua sh. 200 kutokana na mabando ambayo yameisha muda bila kutumika yanaweza kusanya pesa nyingi kwa mwezi sawa na bajeti ya wizara ya habari, mawasiliano na teknolojia ya habari.
Ameitaka serikali kuwasaidia watanzania ili makampuni yaache tabia hiyo kwani amesema mambo ya mabando kuisha muda kwa sasa hayapo katika nchi nyingine duniani.
Akitetea hoja yake amesema kuwa kuna mapendekezo ya kuwa ili kuzuia hilo labda mtu aongeze salio kabla ya muda wa kuisha bando la awali ili kulinda bando lisiishe muda, amesema hiyo si sawa kwani itakuwa ni kumlazimisha mtu kufanya matumizi ya pesa yake ambayo alikuwa hajayapanga ili tu kulinda bando lisiishe muda, amesimamia hoja ya mabando yatumike hadi yaishe na si ku- expire.