Salome Makamba: Uchumi wa Tanzania umesimama tu tangu 2001. Rais haambiwi ukweli na wateule wake

Salome Makamba: Uchumi wa Tanzania umesimama tu tangu 2001. Rais haambiwi ukweli na wateule wake

Makamba alisema tatizo hilo linatokana na uchumi wa Tanzania kusimama tangu mwaka 2001 na kudai wateule wanashindwa kumwambia ukweli Rais ili abadili mfumo wa maisha.
Wenyewe wanasema eti Magufuli ameutembeza mpaka kufika kwenye "uchumi wa kati". Sijui hii dhana ya uchumi kufika level za kati huwa inapimwaje na hawa wataalamu wetu ?
 
Dodoma. Mbunge wa Viti Maalum Salome Makamba aliyefukuzwa Chadema amesema itachukua zaidi ya miaka 60 ili kufikia pato la dola 1,500 kwa mtu mmoja kwa mwaka.

Makamba alisema tatizo hilo linatokana na uchumi wa Tanzania kusimama tangu mwaka 2001 na kudai wateule wanashindwa kumwambia ukweli Rais ili abadili mfumo wa maisha.

Mbunge huyo alitoa kauli hiyo wakati akichangia mpango wa Serikali uliowasilishwa mapema juzi ukionyesha mwelekeo wa bajeti ya 2021/22 ambapo alisema pato la mtu wa kawaida linakuwa kwa mwendo wa kinyonga kutoka dola 1,043 miaka mitano iliyopita hadi dola 1080 kwa sasa.

Hata hivyo, takwimu za Makamba zilipingwa na mbunge wa Vunjo (CCM), Dk Charles Kimei, aliyesema pato la Taifa halipimwi kwa namna aliyoisema kwani kuna mambo mengi yanaangaliwa ikiwemo huduma za umma.

Dk Kimei alisema ni vigumu hukusanyisha mahitaji na kipato cha mtu mmoja mmoja katika mifuko yake kwani Serikali ikifanya hivyo itakuwa inakosea bali kinachoangaliwa ni namna ambavyo watu wanaweza kupata mahitaji muhimu na kisha huchukua pato la jumla kwa nchi wanagawa kwa idadi ya watu ndipo wanazungumzia uchumi ambao alisema haoni shida kwa Tanzania.

“Hali ya uchumi ni mbaya tena mbaya sana, Rais haambiwi ukweli na wachumi wetu, umasikini sasa ni asilimia 26.2 hivyo hatuendi mbele ila tunarudi nyuma, hii itatuchukua miaka 60 kuyafikia malengo ya dola 1,500 kwa mtu mmoja,” alisema Makamba.

Mbunge huyo alishauri kufanyika mageuzi ya kisheria na kisera huku akionya wachumi kuwa kimya na kutomweleza ukweli kiongozi wa nchi kunaweza kuwa mojawapo ya athari hizo.

Alisema mfumo shirikishi ndiyo unaweza kulivusha Taifa kwa sasa pamoja na kuundwa kwa tume ya maridhiano ambayo itakwenda kuwaweka pamoja wananchi ili kutibu makovu ya uchaguzi mkuu kwani wengi wanaona kinyongo hata kutoa fedha zao kulipa kodi.

Kingine alipendekeza kuunda kamati itakayofuatilia ahadi zote za viongozi na viongozi wakuu na kuona namna bora ya kuzisimamia ambapo kutapelekea maisha bora na kuifurahia bajeti kwa pamoja.

Katika hatua nyingine mbunge huyo alipendekeza kupelekwa sheria bungeni itakayoweka mfumo wa ukusanyaji wa kodi ya majengo na vitambulisho vya wajasiliamali baada ya Serikali kuu kuwarudishia halmashauri akisema hakuna sheria ya kuwaongoza wakurugenzi badala yake wataishia kuwapiga akinamama mitaani.

Akichangia kwenye mpango huo, Mbunge wa (CCM), Riziki Lulida aliomba wabunge kuunganisha nguvu zao na kupaza sauti kwenye mambo ya utalii ambao unaweza kuliingizia taifa fedha nyingi.
Tunaomba wabunge wasimamie na kuhakikisha wizara zinazoshughulikia kilimo, mifugo na uvuvi zipewe kipaumbele ili watu tusije kufa njaa, maana yake tunapoelekea Mungu ndiye ajuaye. Basi bora tuwe na chakula cha kutosha hata kama tukikosa maendelo lakini chakula kiwepo siku zisonge mbele.
 
kwamba kwa siku hatumii vocha ya 500, hanunui mafuta ya kula ya 500, hanunui dagaa wa 500, hasagi unga kwa 500, hanunui sukari ya 500 au 1000, hanunui majani ya sh 50, anafikaje kesho huyo bila kula?
Hata huko kwenu usukumani kuna watu hawanywi chai kwa mwezi mzima, dagaa wanazisikia redioni sembuse kununua vocha? Acha kijifaragua wewe?
 
kwamba kwa siku hatumii vocha ya 500, hanunui mafuta ya kula ya 500, hanunui dagaa wa 500, hasagi unga kwa 500, hanunui sukari ya 500 au 1000, hanunui majani ya sh 50, anafikaje kesho huyo bila kula?
Amini nakwambia kuna sehemu nchi hiii...ukimuita mtoto umpe andazi hajui cha kulifanyia,maana hajawahi kuliona.
 
Huyu kakosea mlango wa kuingia... hili bunge ni la sifa na mapambio kwa msukuma.
 
Inakuwaje daktari anashindwa hata kuwekewa oxygen anaposhindwa kupumua mpaka anakufa wakati wabunge ambao hata hawajachaguliwa na wananchi wanachezea kodi za wananchi????
 
Back
Top Bottom