Salon ya kiume

Kaka Kapo

JF-Expert Member
Joined
Nov 23, 2012
Posts
547
Reaction score
344
Ndugu wanajanvi! Nipo katika mchakato wa kufanya biashara ndogo ndogo kwa lengo la kukuza kipato changu apart from kimshahara hiki cha mawazo! Katika kubangua bongo nifanye aina gani ya biashara nikapata wazo la Kuwa na salon ya kiume! Nikafanya utafiti mdogo kwa kuwauliza vinyozi jinsi biashara hiyo inavyooperate! Maelezo yote niliyopata yalikuwa ni ya waajiriwa wa salon na si wamiliki wake! Sasa nimeleta uzi huu maalum kwa wamiliki wa biashara kama hii au yeyote anayejua jinsi biashara hii inaendeshwa na kwa kiwango gani inaweza kutoa faida na pia capital yake yaweza Kuwa kiasi gani? Natanguliza shukrani za dhati kwako ww mchangiaji!
 
Saloon inategemea na population ya hlo eneo,huduma nzuri na mchanganyiko(scrub.wave),wahudumu wazuri pia. Kuhusu faida inategemea na sehemu. Pia umejiandaaje kupata wateja wapya?
Wenye saluni watakuja wajazie
 
Saloon inategemea na population ya hlo eneo,huduma nzuri na mchanganyiko(scrub.wave),wahudumu wazuri pia. Kuhusu faida inategemea na sehemu. Pia umejiandaaje kupata wateja wapya?
Wenye saluni watakuja wajazie
thanks a lot ndugu
 
Ni biashara nzuri mi nilishawahi kuwa nayo miaka ya nyuma na ilikuwa standard san, tatizo lake ni kipato chake kiko fixed sana kama ukikubaliana na kinyozi kwa wiki akuletee 20,000/= basi kama una vinyozi wawili jua kwamba ni 40,000x4=160,000/= kwa mwezi hii itakuwa ni hesabu ambayo ni fixed tofauti na biasahara zingine ambazo siku nyingine inaweza kukutoa kwa dili moja, fanya kwa nia ya kujiongezea mshahara ila si ya kukutoa saaaaana, unless otherwise kinyozi uwe mwenyewe hapo utaiona faida maaana mapato yote utakuwa unakusanya mwenyewe, Na bado vinyozi hawajakuzingua maaana sometime hesabu hawaleti wanakupiga sound watalipa next week nilikuwa na matatizo na kama binadamu huwezi kukataa
 
Ningependa kujua,baada ya kuletewa hizo pesa na vinyozi,pesa ya umeme,maji,vifaa na madawa nani mhusika hapo wa kugharamia??
 
Kwa ujumla biashara ya salon ni nzuri kama ukipata vinyozi wazuri na wasio wasumbufu. vifaa vya salon ni ghali sana, mi nakushauri uende kwanza madukani ukafanye window shoping ya viafaa, then utakuwa kwenye position ya kujua unahitaji capital kias gani.
 
Ka mwenyewe salon..usimwachie MTU.....
Walipe vijana salon..waajiri...usiwakabidhi ofisi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…