Kaka Kapo
JF-Expert Member
- Nov 23, 2012
- 547
- 344
Ndugu wanajanvi! Nipo katika mchakato wa kufanya biashara ndogo ndogo kwa lengo la kukuza kipato changu apart from kimshahara hiki cha mawazo! Katika kubangua bongo nifanye aina gani ya biashara nikapata wazo la Kuwa na salon ya kiume! Nikafanya utafiti mdogo kwa kuwauliza vinyozi jinsi biashara hiyo inavyooperate! Maelezo yote niliyopata yalikuwa ni ya waajiriwa wa salon na si wamiliki wake! Sasa nimeleta uzi huu maalum kwa wamiliki wa biashara kama hii au yeyote anayejua jinsi biashara hii inaendeshwa na kwa kiwango gani inaweza kutoa faida na pia capital yake yaweza Kuwa kiasi gani? Natanguliza shukrani za dhati kwako ww mchangiaji!