Salum Mayanga: Sina upendeleo kwa wachezaji wa Simba

Salum Mayanga: Sina upendeleo kwa wachezaji wa Simba

manyanga ni mjinga,je kuna sbb zipi zinazomfanya mfungaji bora wa msimu uliopita abdulrahman musa wa jkt ruvu,asimuite stars,au sbb atoki Yanga au mikia!
 
Kocha Mkuu wa timu ya taifa ya mpira wa miguu Taifa Stars, Salum Mayanga amesikitishwa na uongo unaoendelea kusambazwa mitandao kuwa anawachukia wachezaji kutoka Yanga huku akiwabeba zaidi wachezaji wa Simba kwenye kikosi chake.

Mayanga amesema taarifa hizo amezisikia tuu kutoka mitandaoni ila hajui wanaomzushia wana ajenda gani dhidi yake kwa hajawahi kuletewa malalamiko na Viongozi wa klabu hizo.

Hizo taarifa nazisikia sikia tuu kutoka kwenye mitandao lakini sijawahi kuletewa malalamiko na kama kuna mtu anasambaza ujumbe huo basi ni chuki tuu, Sina upendeleo kwa wachezaji wa Simba wala Yanga “,amesema Mayanga kwenye mahojiano yake na Radio ABM FM.

Mayanga amesema haijawahi kutokea kupendelea timu moja zaidi ya kuangalia kiwango cha mchezaji husika kwani hata alivyokuwa Kocha msaidizi alimshauri Kocha wa kipindi hicho, Mart Nooij kuchukua wachezaji 9 kutoka Yanga kutokana na uwezo wao kwa kipindi hicho.

Nakumbuka kipindi kile wakati nilipokuwa msaidizi wa Mart Nooij mimi ndiye niliyemshauri tukateua wachezaji 9 kutoka Yanga, Wanayanga waukubali ukweli juu ya kikosi chao, angalia beki wa kati, alikuwa Bossou, kwenye viungo kuna Kamusoko na Niyonzima, wakati safu ya ushambuliaji ni Ngoma, Tambwe na Chirwa, pale nifanyeje kama si kunionea?”,alimaliza Mayanga kwa kuhoji.

Kocha huyo wa Stars amesema kwa kutambua upungufu kwenye safu ya ulinzi, alimuomba Kelvin Yondani aje kuimarisha nguvu lakini beki huyo aliombwa aachwe ili akamilishe kwanza mipango ya ndoa yake.

Mayanga aliongeza kwa kusema kuwa inakuwa vigumu kuwaita Nadir Haroub ‘Cannavaro’, Haji Mwinyi, Salum Makapu na Aggrey Morris baada ya Zanzibar kupata uanachama wa Shirikisho la Soka Afrika (CAF).

Taifa Stars wikiendi iliyopita ililazimishwa sare ya goli 1-1 na timu ya taifa ya Rwanda mchezo uliopigwa kunako dimba la CCM Kirumba.

Chanzo: Bongo5
Kocha hana kiwango cha kuwa kocha mkuu wampe puljin wa singida united timu imetwaa ubingwa harafu wachezaji akuna timu ya taifa ndio nn sasa

Unaweza hata ukaangali ncbi za wenzetu timu iliiotwaa ubingwa ndio inatoa wachezaji wangi timu ya taifa

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mapovu haya yote ni kwa vile stars haikufanya vzr ila kama ingeshinda watu kimyaa...kocha unansfas ya kumwongeza mchezaji kama abdurhaman wa jkt pamoja na kelvin sabato. Afu pia sion sababu ya kumchezesha msuva na kichuya wakati mmoja. Hawa wachezaji wanapaswa wagombanie namba mmoja aingie kama supper sub...kocha inabd awe mjanja kidogo maana hata sub zako unazofanya hazisaidii team. Tunaumia bure nashaur pia kocha wa kagera sugar aitwe aongeze maujuz kwenye team

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Huyu kocha bwege sana,unaacha washambuliaji wa maana unamchua John Boko? kama sio upuuzi ni nini?
Umeona mchezaji alikuwa injury kitambo harafu unampanga timu ya taifa unataka nn kama sio kuiua timu wacha ikatolewe Rwanda kesho kutwa
Bocco hata timu yake hajaisaidia chochote imeishia nafasi ya nne leo unamweka kushambulia si upuuzi

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Simba Stars na Akili mbovu za Mashabiki wa Yanga.....
1:Kakolanya....Huyu aliitwa ila amekuwa majeruhi na pia asingeweza kuchukua namba mbele ya Manula.
2:Juma Abduli....ni mzuri ila uwezo wake kwa sasa umeshuka sana huwezi kumlinganisha na kapombe....
3:Hajji mwinyi....Yanga wenyewe hawamwamini ndio maana wanataka kumsajili Gadiely michael sasa kama nyie Yanga hamumuamini kijana wenu mnataka mayanja amwamini...?
4:Yondani....Jamaa ameshuka kiwango huwezi kumuacha Nurdin chona....Salum Mbonde na Erasto nyoni kwa ajili ya Yondani
5:Canavaro....Amestafu timu ya Taifa angekuepo nadhani hata mimi ningegundua matatzo ya mayanja.
6:Makapu....Kama ameachwa mkude Ndemla kaitwa juzi na hajatumiwa mnataka Makapu aitwe wakati kiungo bora wa chini ambaye ni mkude kaachwa....akili zenu mbovu
7:Mwashiuya....Unaanzaje kumuita mchezaji anayesugua benchi ukamuacha mtu kama Kichuya...?
8:Emmanuely martini....Yanga anasugua Benchi timu ya nani ya Taifa inayowaita wasugua Benchi..?
9:Kaseke....huyu kijana ni mchezaji mzuru sana lkn amemuharibu Lwandamila kwa kumsugilisha Benchi
10:Matheo Antony....Yanga wenyewe mnajua kuwa huyu ni Garasa
11😛ato Ngonyani.....Yanga wenyewe mnamtema je mnataka Mayanga amuite timu ya Taifa amuache mzamiru Yassin
12:Ibrahimu Ajibu....Ameachwa akiwa bado yupo Simba
.....Hv nyie vyura Mkude....Ndemla na Mo Ibrahimu wangekuwa wachezaji wenu alafu waachwe c Mungemuua Kocha nyie.....
Mnataka tuwaite Chirwa...Ngoma...Bosou...Tambwe na Twite..?
Acheni fikra mgando nyie Gongowazi.
 
Back
Top Bottom