veyra
Member
- Aug 31, 2025
- 19
- 29
Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupita Chama cha Ukombozi wa Umma (CHAUMMA), Salum Mwalim amesema Serikali yake ikiingia madarakani itahakikisha inaboresha huduma mbalimbali yakiwemo maboresho ya sera ya habari ili vyombo vya habari vifanye kazi kwa weledi na kuifanya tasnia hiyo kuwa mhimili kamili kama ilivyo Mahakama, Serikali na Bunge.
Mwalim amesema hayo mkoani Dar es Salaam, wakati wa uzinduzi wa kampeni za uchaguzi za CHAUMMA leo Agosti 31, 2025 na kuongeza kuwa akiwa kama mwanahabari atahakikisha upatikanaji wa habari unakuwa na wigo mpana ili kuibua changamoto za jamii ambazo Serikali yake itazitatua.
Akizungumzia sekta ya kilimo, Mwalim amesema Serikali yake itahakikisha inaongeza nguvu kwenye sekta hiyo ili kuongeza uzalishaji wa chakula na kuwezesha kuwa na uhakika wa chakula na mazao ya biashara.
Katika eneo la utumishi wa umma amesema atahakikisha nidhamu kwa kila mtumishi na kuwaboreshea maslahi yao kwa kuanza na msharaha wa 800,000 kwa kima cha chini, ikiwa ni baada ya makato ya kodi.