GE2025 Salum Mwalimu: CHAUMMA hakuna atakayenyanyaswa kwa sababu ya uraia

GE2025 Salum Mwalimu: CHAUMMA hakuna atakayenyanyaswa kwa sababu ya uraia

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025

DuaZaMama

JF-Expert Member
Joined
Jun 2, 2025
Posts
1,882
Reaction score
4,153
​
Chama cha Ukombozi wa Umma (Chaumma) kimewaahidi wananchi mkoani Kagera na maeneo mengine ya mipakani kuwa, kikipata ridhaa ya kuongoza dola, kitahakikisha hakuna raia anayebughudhiwa au kunyanyaswa kwa sababu ya uraia.

Chama hicho kimesema kitaunda Serikali itakayothamini rasilimali watu kwa maendeleo ya Taifa, kama ilivyo kwa mataifa ya China na Marekani, yaliyo mstari wa mbele kujali rasilimali watu kama msingi wa kupiga hatua kimaendeleo.

Ahadi hiyo imetolewa leo, Septemba 19, 2025, na mgombea urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa tiketi ya chama hicho, Salum Mwalimu, alipozunngumza na wakazi wa Nyakanazi, Wilaya ya Biharamulo, mkoani Kagera.

Mwalimu ameeleza kusikitishwa na namna ambavyo baadhi ya raia wanaoishi maeneo ya mipakani, hususani Kagera na Kigoma, wanavyonyanyaswa kwa tuhuma za uraia, hali aliyoeleza kuwa ni ukiukwaji wa haki za binadamu.

“Tunahitaji rasilimali watu katika sekta kama vile kilimo na ufugaji. Nikichukua nchi, hakuna atakayesumbuliwa kwa sababu ya uraia. Kama si Mtanzania tuambie, kama ni Mtanzania tuambie. Watakaoamua kubaki nchini watapewa vitambulisho vya uraia ili wachangie maendeleo ya Taifa,” ameahidi.​


 
Kumbe GIA ya kuondokea si ile ya Safari . Jamaa walianza kwa mbwembwe nyingi Sana kuivuruga chadema.
 
Back
Top Bottom