Mkalukungone Mwamba
JF-Expert Member
- Aug 29, 2022
- 3,141
- 7,205
Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Chama Cha Ukombozi wa Umma (CHAUMMA) Salum Mwalimu amesema kuwa endapo atapata ridhaa ya kuongoza nchi, Serikali yake itabeba gharama zote za timu itakayoshiriki Michuano ya Klabu bingwa Barani Afrika.
Akizungumza leo katika Viwanja vya Biafra viliyoko Kinondoni Dar es saalam Salum amesema Klabu za Tanzania zimekua na kasumba ya kutofanya vizuri kwenye michuano hiyo kutokana na Changamoto mbalimbali ikiwa ni pamoja na uchumi.
Amesema endapo atapata nafasi ya kuwa Rais wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania atahakikisha Klabu yoyote kutoka nchini inachukua ubingwa wa michuano ya Klabu bingwa Barani Afrika na kuling’arisha soka la Tanzania Kimataifa.