GE2025 Salum Mwalimu: Naiona hatari ya kazi ya bodaboda kuzidiwa na itakuwa si msaada tena

GE2025 Salum Mwalimu: Naiona hatari ya kazi ya bodaboda kuzidiwa na itakuwa si msaada tena

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025

Richer

JF-Expert Member
Joined
Jun 9, 2025
Posts
2,318
Reaction score
4,079
Mgombea urais wa Chama cha Ukombozi wa Umma (CHAUMMA), Salum Mwalimu, amesema kuwa licha ya pikipiki za biashara maarufu kama bodaboda kuwa mkombozi wa ajira kwa vijana wengi nchini, ipo hatari kubwa sekta hiyo kupoteza maana kama suluhisho la ajira endapo serikali haitatafuta mbadala wa kudumu wa ajira.

Akizungumza kwenye moja ya mikutano yake ya kampeni, Salum Mwalimu alisema kuwa kwa sasa bodaboda imekuwa kimbilio la kila kundi — vijana, wastaafu, watumishi wa umma, na hata wale walioajiriwa — hali ambayo inatishia uendelevu wa biashara hiyo

“Ninawaambia, baada ya miaka michache ijayo, bodaboda itakuwa siyo tegemeo tena kama ilivyo sasa. Kila mtu ana boda — wasomi, wastaafu, hata waliokuwa na ajira. Mwisho wa siku, zitakuwa nyingi kuliko abiria, na hazitakuwa msaada tena,” amesema Mwalimu
Amesema kuwa ingawa sekta ya bodaboda imechangia kwa kiwango kikubwa kusaidia watu kujipatia kipato, haitakiwi kuwa suluhisho pekee la serikali katika kukabiliana na tatizo la ajira

“Hii ni hatari, na kama taifa, tukiruhusu hali hii iendelee bila kutengeneza fursa nyingine za ajira, tunatengeneza bomu la kijamii,” ameongeza

Mwalimu ameahidi kuwa endapo chama chake kitaaminiwa kuunda serikali, ataweka mkazo katika kutengeneza fursa nyingi za ajira endelevu, hasa kwa vijana, kupitia uwekezaji katika viwanda, kilimo cha kisasa, na teknolojia.

“Vijana wetu wanahitaji zaidi ya pikipiki — wanahitaji fursa za kiuchumi zinazowapa matumaini ya maisha bora,” amesema Mwalimu, akihitimisha hotuba yake kwa wito wa mageuzi ya kiuchumi yatakayolenga kuondoa utegemezi wa bodaboda kama suluhisho la ajira nchini

1761228595788.png


Chanzo: Nipashe Digital
 
Sio baada ya miaka michache ijayo..tayari zishajaa..wanakaa tu maskani abiria wa kugombea
 
Back
Top Bottom