Mtiania urais wa Tanzania wa Chama cha Ukombozi wa Umma (Chaumma), Salum Mwalimu ameendelea kuzunguka mikoani kutafuta wadhamini ili kumwezesha kuteuliwa na Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC) kuwania urais katika uchaguzi mkuu utakaofanyika Jumatano, Oktoba 29, 2025.
Mwalimu ambaye pia ni Katibu Mkuu wa Chaumma, leo Jumanne, Agosti 19, 2025 amefika stendi ya zamani ya Iringa Mjini kusaka wadhamini hao ambapo amewaambia akifanikiwa kushinda na kuwa Rais: “Nitavaa kapelo, tisheti na jeans mtaa kwa mtaa kuchapa kazi."
Kwa mujibu wa Sheria ya Uchaguzi wa Rais, Wabunge na Madiwani ya mwaka 2024, kifungu cha 33 (1) kinaeleza: Ili kuweza kuteuliwa kuwa mgombea halali wa kiti cha Rais, mtu anapaswa kudhaminiwa kwa maandishi na wadhamini walioandikishwa kuwa wapiga kura kwa madhumuni ya uchaguzi chini ya sheria hii wasiopungua 200 kwa kila mkoa, angalau kwa mikoa 10 ya Jamhuri ya Muungano, kati ya hiyo angalau mikoa miwili kutoka Zanzibar.