GE2025 Salum Mwalimu: Nikiwa Rais, nitavaa kapelo, Tisheti na Jeans Mtaa kwa mtaa

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025

Richer

JF-Expert Member
Joined
Jun 9, 2025
Posts
2,318
Reaction score
4,079
Mtiania urais wa Tanzania wa Chama cha Ukombozi wa Umma (Chaumma), Salum Mwalimu ameendelea kuzunguka mikoani kutafuta wadhamini ili kumwezesha kuteuliwa na Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC) kuwania urais katika uchaguzi mkuu utakaofanyika Jumatano, Oktoba 29, 2025.

Mwalimu ambaye pia ni Katibu Mkuu wa Chaumma, leo Jumanne, Agosti 19, 2025 amefika stendi ya zamani ya Iringa Mjini kusaka wadhamini hao ambapo amewaambia akifanikiwa kushinda na kuwa Rais: “Nitavaa kapelo, tisheti na jeans mtaa kwa mtaa kuchapa kazi."

Kwa mujibu wa Sheria ya Uchaguzi wa Rais, Wabunge na Madiwani ya mwaka 2024, kifungu cha 33 (1) kinaeleza: Ili kuweza kuteuliwa kuwa mgombea halali wa kiti cha Rais, mtu anapaswa kudhaminiwa kwa maandishi na wadhamini walioandikishwa kuwa wapiga kura kwa madhumuni ya uchaguzi chini ya sheria hii wasiopungua 200 kwa kila mkoa, angalau kwa mikoa 10 ya Jamhuri ya Muungano, kati ya hiyo angalau mikoa miwili kutoka Zanzibar.


Your browser is not able to display this video.
 
 
Huyu ndio angekuwa Makamu wa Rais Tundu Lisu 2020

Chadema ndio sababu Shujaa Magufuli aliidharau sana 🐼
 
Mambo ya hovyo hovyo tu!!
 
Akiwa Iringa Mjini leo, Salumu Mwalimu mgombea urais CHAUMMA amesema: "Mimi mkinichagua nitavaa suti siku ya kuapishwa, siku ya kuzindua bunge na siku ya kupokea Marais kutoka nchi nyingine, lakini zaidi ya hapo ni tisheti na jinsi kuingia mtaa kwa mtaa kutatua matatizo ya wananchi, nitawatumikia usiku na mchana."

 
Kwa nini asivae sasa hivi apite mtaa kwa mtaa asake kura. Kwa nini asubiri mpaka achaguliwe kuwa raisi ndio aje avae hivyo.

Mwaka huu tujiandae kusikia na kuona mengi. Mpaka kufika oktoba tutaona na kusikia mengi.
 
Kweli u-Rais sasa limekuwa jambo rahisi...!!
Yupo mwingine sera yake ni kuondosha vitanda vya 6 kwa 6 majumbani...!
Hahahaaa! Tutasikia mengi mwaka huu.kwahiyo baada ya kushiba ubwabwa ana vaa tisheti na jinsi.
 
CHADEMA walitukosea sana mwaka 2020 ,kumuweka huyu Jamaa Kama mgombea mwenza.
Imagine,huyu Jamaa angekuwa ndiye Makamu wa Rais sasahivi endapo CHADEMA ingeshinda mwaka 2020.
 
Huyu mtangazaji wa channel ten anafikiri Watanzania ni wajinga kumchagua 'comedian'
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…