GE2025 Salum Mwalimu: Nitamwaga Matrekta mtaacha kazi ya Boda Boda

GE2025 Salum Mwalimu: Nitamwaga Matrekta mtaacha kazi ya Boda Boda

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025

DuaZaMama

JF-Expert Member
Joined
Jun 2, 2025
Posts
1,882
Reaction score
4,153
Sera za Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Chama cha Ukombozi wa Umma CHAUMMA Salum Mwalim Akiwa Nyakanazi, Biharamulo mkoani Kagera, wakati akielekea mkoani Kigoma, ameahidi mageuzi makubwa katika sekta ya kilimo.

Amesema, endapo atachaguliwa kuwa Rais, atahakikisha anaimarisha kilimo kwa kusambaza matrekta na pembejeo za kisasa kwa wakulima nchini ili kuongeza uzalishaji na kuwawezesha vijana kuachana na ajira zisizo na tija kama bodaboda.

Ameongeza kuwa kilimo kitakuwa nguzo ya ajira na uchumi wa taifa, na serikali yake itaweka msukumo mkubwa kwenye masoko na teknolojia za kisasa za kilimo.
 
Back
Top Bottom