McLaren
JF-Expert Member
- Feb 19, 2025
- 1,170
- 3,743
Katibu Mkuu wa CHAUMMA Salum Mwalimu akizungumza leo amesema kuwa Tume ya Taifa ya Uchaguzi inapaswa kutoa ufafanuzi zaidi kuhusu sababu zinazochangia vitendo hivyo vya utekaji ikiwa ni pamoja na sababu za kisiasa.
Alibainisha kuwa hadi sasa, sababu zilizotajwa ni mapenzi, biashara, na visasi pekee, jambo ambalo limezua mjadala mkubwa miongoni mwa wananchi
"Kuna masuala ya utekaji. Tunadhani Tume ingekwenda mbali kidogo kueleza na sababu nyingine ambazo zinatengenezewa hisia kwenye jamii, ikiwemo sababu za kisiasa.
Na labda wanazo, na sisi tunatoa rai kwa Tume; kama wana sababu nyingine waseme. Lakini pale walipoishia, ndiyo maana mjadala umekuwa mkubwa. Kwamba utekaji ni mapenzi tu, na biashara tu, na visasi tu.
Tunadhani labda zipo na sababu nyingine, kwa hiyo wangekwenda mbali zaidi pengine kuchunguza. Tunaelewa wao wameegemea taarifa za polisi pekee yake kama ambavyo wamesema.