TANZIA Salum Shamte wa Katani Ltd afariki dunia


Ni jambo la kusikitisha kuwa Bwana Shamte amekufa akiwa "mfungwa" ambaye hakuwa amepata nafasi ya kujitetea ....ili kuongea upande wake mahakamani, tumesikia habari za upande mmoja ambazo ndio kama zilikuwa zimemuhukumu .....amekufa akiwa bado yuko ndani kwa makosa ambayo hayana dhamana na ilibidi kupelekwa pale na Magereza kwakua bado alikuwa kizuizin

KOSA LA SHAMTE NI KUWA MWENYEKITI WA TPSF ....ALIKUWA AMESHAONYESHA WAZI KUWA HAMTAKI NA ALITUMIA NJIA HIYO KUMUONDOA ...KWA MUDA WOTE AMBAO SHAMTE AMEKUA MWENYEKITI WA TPSF ...AMEKUWA AKIRUKWA KWENYE MAMBO MENGI YA KIKAZI TOKA JUU NA BADALA YAKE AMEKUWA AKITUMIWA MAKAMU WAKE ...AMBAYE "WANAONGEA LUGHA MOJA" ....NA NDIYE AMEKUWA AKIPELEKA MANENO YOTE YA UCHONGANISHI YALIYOFANIKISHA SHAMTE KUPINDULIWA PALE KWA HIYO KESI ILI ASIWE KIONGOZI WA WAFANYABIASHARA
 
Watenda dhambi tuu wengi... basi tujichunge tusihukumu nasi tusije hukumiwa!!
Pole kwa walioguswa nasi tunamtakia kheri aistahiliyo huko aendako...
 
Apumzike kwa amani
 
Pole
 
Dau hawamwezi

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Poleni sana kwa yote.

Hivi wewe na "mentor" wako mlishindwa nini kusajili na kupata hati ya "hakimiliki" za uvumbuzi uliotokana na tafiti zake, hapo BRELA?
 
Tutaiba, tutadhulumu, tutafanya yooote, mwisho wa siku tunaondoka tukiwa watupu tunarudi Mbinguni kwa Mungu aliyetuumba.

Twendeni kwa tahadhari.

Pumzika Shamte!

Sent using Jamii Forums mobile app

Kwa hiyo Shamte kaiba na kadhulumu??????, mie namuona kama shujaa aliyekatishwa uhai na utawala wa kidhalimu wa mtukufu Jiwe. Shamte ni victim mwingine wa udikteta na utawala wa kimabavu usiozingatia utawala wa kisheria.

Mnawaweka lumande washua kwao ni zaidi ya Kifo manake hawajazoea taabu, sononi lazima iwaue na ukichanganya na umri ndio kabisa. Hapa sasa Jiwe na wafuasi wake roho kwatu.
 
Mungu ndiye ajuaye hatima ya kila mmoja, tuishi tukifahamu kuna kuondoka. Tujiweke tayari.
Kujiweka tayari ndilo tatizo mkuu 'Kwemdimu'; hasa ikijulikana wazi kwamba "Mungu ndiye ajuaye hatma ya kila mmoja...."

Hata ujiweke tayari vipi, kama "hatma" ilishapangwa ni kazi bure.

Mungu amweke mahali pema Mzee Shamte. Hakuna ajuaye, yeye alishapangiwa wapi. Sisi tunakisia tu, "pawe mahali pema."
 
Innallillah wainallillah rajiun.
huwa mtu akituhumiwa kwa ufisadi bongo natabasamu na kusema ametolewa kafara tu sababu sina ushahidi ila kwa vile nchi yetu ni maskini mimi naamini we have numerous mafisadi kila kona wengine wafa wengine wako imara ambao ni chui walio na ngozi ya kondoo tukiwasifu kwa nyimbo na mapambio na vigelegele kwa kuwa wana bahati ufisadi zao hazijaanikwa na hatuwajui!! kaburi tu ndio kiboko ya fisadi na halikwepeki kwa mlungula! tena ukiwekewa kaburi la zege hutoki hata ikitokea bahati umeyashinda mauti just one hour after watu waliokuzika kutawanyika!
 
Tutaiba, tutadhulumu, tutafanya yooote, mwisho wa siku tunaondoka tukiwa watupu tunarudi Mbinguni kwa Mungu aliyetuumba.
Eeee!

Kama ni hivyo nami kesho naanza kazi: "nidhurumu, nifanye yoote" mazuri na mabaya mradi najua "nitarudi Mbinguni kwa Mungu."

Shida ipo wapi hapo?

Na mara nyingi 'kudhurumu na kufanya mabaya' hulipa haraka sana, kuliko kutegemea malipo kwa yale mazuri unayotenda.
 
Fanya yote usisahau hata moja.
Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…