Mangungo II
JF-Expert Member
- Jul 6, 2012
- 18,133
- 26,766
Nagojea Taazia ya mzee mohamedsaidi.Nenda mwanakwenda Shamte. Ulimdhulumu sana Uncle wangu, akawa demoted, wewe na akina Marehemu Ibrahim Kaduna, mkamfanya aishi maisha magumu na ya stress sana. Mkadhulumu haki miliki za tafiti zake, aligundua jinsi ya kutengeneza pombe kwa kutumia maji ya mkonge, chakula cha kuku kwa kutumia mabaki ya mkonge na umeme kwa kutumia maji maji ya mkonge.
aliandika vitabu kuhusu mkonge lakini hakufaidika navyo. Alinieleza haya 2007 na mwaka huo huo akapata stroke, nilimuuguza Tanga, mkashindwa kumlipia hata Ambulance kutoka Tanga to Muhimbili.
nilipowatafuta kwa ajili ya matibabu yake mkaishia kunipa Tzs 50,000. Mzee Shamte unakumbuka siku ile uliniita pale fire? Ukampa dereva bahasha yenye hio pesa?
Baadae ali-recover bado mkagoma kumlipia bill, na MKUMBUKE alistahili sio kwamba ilikua fadhila.
Siku moja jioni ya 12 tukiwa tumerudi kutoka kwenye mazoezi ya viungo pale Morocco Physiotherapy clinic, STARTV wakawa wanaonyesha kipindi cha mkonge na walionyesha hizo products ambazo huyu mzee wangu ndio alikua amwzifanya yeye ila zilitangazwa kama vile ni kazi iliyofanywa na mtoto wa Shamte. Kwakuwa nilikua nine Shaun vanish a dots, nikachukua remote nikataka kubadili Chanel, ananiambia nisiondoe.
Next day akiwa kwenye mazoezi napata second stroke na ndio ikawa mwisho wake. Akina Shamte bado walishindwa hata kumsafirisha.
sina nia mbaya, kifo ni kifo but kwa kusema haya naamini nimemtendea haki Marehemu Mentor wangu. He was a true friend of Mine.
Muislam bilionea amefariki lazima atie neno ,wapi alikutana nae iwe msikiti wa mtoro au pale tanga mjini
Na mchango wake katika uislamu
Apumzike anapostahili
Sent using Jamii Forums mobile app