Salute Kwao Popote Walipo.

Cytochrome p450

JF-Expert Member
Joined
Mar 19, 2019
Posts
5,638
Reaction score
15,044
Acha nianze kwa kutoa SALUTE kwao!

Kuna wanaJF waliotumia akili nyingi sana kufungua threads ambazo baadhi zina mwendelezo na nyingine ni Non-Stop, unless ziondolewe!

Ningependa ni-point out threads zangu tano (5) ambazo naamini waliozishusha basi walizisuka ipasavyo.. (Unaweza kushusha nawe list yako hapo chini)

1. Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate likes.

Nimeona hii thread iwe #1 kwa upande wangu.
Humo hata ukiweka emoji ya dole la kati, likes zako ziko pale pale zinakufuata. Halafu hakupoi, muda wote kumewaka!

2. Wa mwisho ndio mshindi.

Huwa najiuliza sana huyu jamaa aliwaza nini mpaka akashusha uzi kwenzi namna hii.. Hahaa noma sana!

Huu uzi hautokuja kuisha labda atake Mungu.
Nakumbuka kuna siku niliingia online saa 9 za usiku nikatuma ujumbe wa mwisho angalau niwe mshindi mpaka asubuhi, kuna mdau sijui alitokea wapi akaongeza jumbe zingine chini yake. Hhhm! Dah!!

3. Usichukulie poa, nyumba ni choo.

Mhhh mhhh!!
Kwa wale wenzangu na mimi wa kupenda vijungu.
Humu ndani utakuta vyoo vya kisasa.
Mizigo kama hii..

...ni kawaida sana kuikuta. (Sijasema ukaicheki)

4. JamiiForums Usiku wa manane.

Mapopo humu utawakuta. Yani wee ukijiona umeshtuka saa 8 za usiku na huna usingizi labda unataka kuchat, wee ingia tu humo. Utapata kampani la kutosha tu.

5. Uzi maalum kwa ajili ya vyakula.

Sijui ndio ulivyoandikwa hivyo?!

Ila ndio hivyo bhana, humo mambo ya misosi mazaga zaga ndo penyewe.
Ushindwe wewe tu!

Acha nikomee hapo. Kama unayo list yako ya thread unazozikubali embu jaribu kushare nasi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…