Salvatory Edward Vs Shekhan Rashid


Unamuwekaje Boban kundi moja na Fei Toto?
 
Kwa wale wapenzi wa soka wa zamani, umepewa nafasi ya kuchagua mmojawapo ili kikosi chako kitimie, kati ya Shekhan na Salvatory nani unampa nafasi katika timu yako?

Kwa bahati nzuri wote nimewaona ( nimewashuhudia ) japo Mmoja wao Shekhan Rashid niliwahi Kucheza nae ' Kimtaa ' pale Uwanja wa Uhuru Mchanganyiko katika Timu ya Shaurimoyo ila kwa Salvatory Edward sikuwahi. Hata hivyo pamoja na ' Usimba ' wangu lakini kwa Wawili hawa nitawachambua ' Kimpira ' zaidi na kamwe si Kishabiki.

Salvatory Edward alikuwa ni Kiungo ' too direct ' and ' attacking minded ' Kiuchezaji na alikuwa na ' Mapafu ' ya kweli ya Kuichezesha Timu yake ya Yanga SC vizuri sana enzi hizo akishirikiana na mwenzake Waziri Mahadhi ' Mendieta ' wa Tanzania na si ajabu Yanga SC yao ya wakati huo ilikuwa ipo Moto sana. Na nilichompendea zaidi Salvatory Edward ' Mtaalam ' ni Nidhamu yake na sikumbuki kama hata alishawahi kuonyeshwa Kadi Nyekundu katika ' Career ' yake akiwa na Wapinzani wetu Wakubwa Yanga SC. Uwezo mwingine mkubwa aliokuwa nao Salvatory Edward ' Mtaalam ' ni ule wa Kupiga Mashuti ( Mawe ) ya mbali ambayo mengi yalikuwa yakiingia ipasavyo. Alikuwa ni Kiungo wa Kazi Kazi.

Shekhan Rashid alikuwa ni Kiungo ' very tactful, versatile and multi talented ' hasa katika Kiungo cha Juu. Alikuwa anajua Kuiendesha Timu vyema, kupanga Mashambulizi na kupiga Pasi ' Mpenyezo ' za hatari ambazo zilikuwa zikiwafanya Washambuliaji wa Simba SC akina Machupa na Gabriel ' Batigol ' wawe wanacheka tu na nyavu wakati wote huku nyuma yake Shekhan Rashid akiwepo Kiungo wangu bora na wa muda wote wa Chini na Nahodha wangu mwenye Mafanikio na Simba SC Seleman Abdallah Matola a.k.a Mzambia a.k.a Veron. Kasoro yake kubwa Shekhan Rashid na hii alikuwa nayo tokea tukicheza Soka la ' Mtaani ' pale Uhuru Mchanganyiko Shuleni na Timu ya Shaurimoyo ni ya kutokuwa na Pumzi ya kutosha na kuwa ' Nyoro Nyoro ' mno. Alikuwa ni Kiungo wa Ubishoo Ubishoo,

Wote niliwapenda na walikuwa ni burudani tosha Uwanjani enzi zao huku Mmoja Wao akiwa Yanga SC na mwingine Simba SC.
 
Lakini si aliondoka simba 2005 akaenda Denmark huyo Slavatory aliwahi kutoka hata kwenda Kongo tu ?

Sent using Jamii Forums mobile app
 

Hapo.kwenye daraja la juu ongeza na MKUDE ili uonekane una busara
 
Lakini si aliondoka simba 2005 akaenda Denmark huyo Slavatory aliwahi kutoka hata kwenda Kongo tu ?

Sent using Jamii Forums mobile app

Siyo wote wanaoenda nje na kupambwa magazetini, basi wanaenda kucheza soka. Na hata wanaopata bahati ya kucheza soka nje siyo kipimo kuwa, wao ni bora sana kuliko ambao hawakwenda nje.

Kuna mtu aliyekuwa akiitwa Peter Nkwera, huyo jamaa ni namba mbaya mnoo. Siyo Salva au Shekhn walikuwa na uwezo hata kumkaribia tu, matokeo yake aliishia kucheza Reli, majeruhi yakamwandama. akatoka kwny soka
P. Nkwer, Salva wote watoto wa temeke walicheza pamoja...!
 
Thesis yako ni batili huwezi kumlinganisha mtu aliyeshindwa Kufika mbali kwa sababu ya Majeraha na mtu ambaye hakusumbuliwa na majeraha..

Ningekuelewa kama ungesema Salvatory alikuwa bora ila akiamua kucheza soka la ndani na Shekhan aliamua tu kwenda huko.

Haya uliwezaje kupima kiwango cha huyo Nkwera wakati alikuwa injury prone?

Sent using Jamii Forums mobile app
 

Salva, Nkwera na Lunyamila wote walicheza umiseta wanajuana tangu shule. Lunya alichezea shule ya mikoani nadhani shinyanga

Kiwango kikubwa cha Peter, ilifanya timu ya Reli ya Moro imlipie ada O level, na alipo maliza alienda kujiunga nayo. Kumbuka Salva na Petr ukiacha mtaani, pia walimaliza shule moja olevo.

Ilimchukua Salva miaka miwili mbele ili kucheza daraja la kwanza, wakti petr na lunya walikuwa tayr, akaenda sigara na Lunya yanga..

wengine wanaenda ulaya kutokana na connection tu walizonazo, na wapo wazuri hawaendi kutokana na sababu kadhaa nyuma yao..
 
Ok sawa.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Salvatory alikwenda kucheza Oman, uturuki .Uturuki alipata timu Ila alikuta dirisha limefungwa la usajili aka fanya majaribio akawa amefuzu tena timu ya wakubwa. Ishu ikaja Yanga Waka mtaka ajiunge ili ashiriki club bingwa Afrika, Aka amua aachane na kusubiri msimu wa usajili Ulaya akaja kusajiliwa Yanga.

Salvatory, Peter Nkwela na mwingine nime msahau wote walitokea Kibasila Secondary kwenda timu ya Umiseta mkoa wa Dar. Ila Salva alicheza Cargo, Sigara, Yanga.Peter Nkwela alikua akicheza namba tano na si namba nane.


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mimi mdau wa Simba SC .
Salvatory alikuwa mtu kazi haswa ila Shekhan alikuwa ni wale viungo wa udambwi udambwi . Kwahiyo inategemea unapenda kuona nini kwa mchezaji .Kama ni majumuisho ya jumla Salva yuko juu ya Shekhan kutokana na tofauti ya kujitambua , ila wote walikuwa na vipaji asilia
Kwa wale wapenzi wa soka wa zamani, umepewa nafasi ya kuchagua mmojawapo ili kikosi chako kitimie, kati ya Shekhan na Salvatory nani unampa nafasi katika timu yako?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hawachelewi kumlingamisha Salum Machaku na SMG hawa....
 
Hiz Salva alikuwa mtu zaidi ya shekhan Rashidy
Lakini hizo stori za uturuki sijui dirisha kakuta limefungwa ni stori ambazo wachezaji wote wanajificha kwenye kimvuli hicho
Salva alishindwa kucheza moira uturuki akazuga zuga kidogo akarejea Tz kuendelea kucheza Yanga


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…