Sam Misago, kwa hili ulilomfanyia Shetta umejishushia hadhi

ESPRESSO COFFEE

JF-Expert Member
Joined
Sep 6, 2014
Posts
6,170
Reaction score
7,665
Nimekuwa nikifuatilia sana hiki kipindi cha Friday Night Live kinachorushwa kila Ijumaa ya wiki usiku na Sam Misago. Kumekuwa na interview za wasanii mbalimbali lakini nimegundua hiki kipindi ni jipu kwa wasanii wetu!!!

Anachokifanya Sam ni ujinga wa hali ya juu ambao hauwezi kuvumilika! Kama kuna wadau wengine huwa wanafuatilia hiki kipindi mtakuwa mmegundua na kuona nini kinachoendelea!!

FNL ya juzi kama uliona Shetta alikuwa ana interview kwenye hicho kipindi na Sam lakini Sam alionesha kutomkubali kabisa Shetta kutokana na maswali aliyokuwa anamuulizaa! Swala la EATV Awards, Sam alionekana kumkandia sana Shetta na kuonesha waziwazi kuwa katika vipengele alivyopo Shetta ni kama hawezi kuchukua tuzo kwa sababu fulani yupo! SHAME ON U SAM!

Wewe ndiye unayeamua mshindi au kura ndo zinaamua? Na kama mnajua fulani ndo atakuwa mshindi, ya nini kuweka usiku kwanini msimpe Tuzo aendeee? Kwanini kuna mashindano?

Shetta alipoteza kabisa 'mood' juzi kutokana na Sam. Kwa walioona watakuwa mashahidi wa hayaa. Sijui ni kukosaa taaluma ya utangazaji au la, lakini hii sio maara ya kwanza kwa Sam. Nakumbuka kuna siku Harmonize alikuwa na Interview FNL, Sam alikomaa na Swala la Harmonize kumuiga Diamond hadi Harmonize akapanic maana anajibiwa lakini interview nzima ni kama alimuitia kumuuliza hilo swalii!

Sam na FNL yake sio hayoo tu, yapo mengi lakini kwa hili la juzi ni wakati wa wasanii sasa Kukisusia hiki kipindiii kwa alivyofanyiwa Shetta!!! Na kwa maswali yale, ningemuomba Shetta kiutu uzimaa ajitoe kabisa katika kuwania tuzo hizi za AETV awards!! Maana aliabishwa kuwa hawezi shindana na Mwafulani!!!

Sam kama upo hapa na unasoma haya au jamaa ake yeyote wa karibu amfikishie taarifa nafikiri kungekuwa kuna kupiga simu kipindi cha juzi Sam angekoma!! Utangazaji bila taaluma matokeo yake ndo hayo.

 
Maswali ya sam ndo yanafanya watu kukipenda na kipindi kimekuw maarufu japo si vema kumwambia mtu ukweli sheta hawez kushinda hiyo tuzo kuna watu wachache ndo mnaoponda hata mtv pia huwa wanapost picha za mshiriki mmoja mmoja na kuandika chochote
 
Kuna kipindi cha kimbea mbea muda kama huo wa FLN basi uwe unajiunga nao.
 
NAKUBALIANA NA MTOA MADA KWA 100%

Nilitaka pia kulizungumzia hilo. Sam Misago huwa anaangalia wasanii.

Anawaignore na kuwadiss baadhi ya wasanii kisa hawana majina makubwa, badala awapromote hao na kuwapa shavu wenye majina.

Tatizo lake ni kwamba hajasomea utangazaji kwasababu angekuwa neutral.

Sam Misago jirekebishe.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…