Sam Misago, kwa hili ulilomfanyia Shetta umejishushia hadhi

Sam Misago, kwa hili ulilomfanyia Shetta umejishushia hadhi

Namshauri atafute style yake kama anavyofanya rayvan
Mkuu swala la kufanana sauti plus style kwenye mziki ni kitu cha kawaida kutokea. Na ndio maana hakuna kesi iliyowahi kufunguliwa kuhusiana na hizo mambo. I bet utakua unawajua Future na Disigner(Panda) .. Hawa jamaa wanafanana karibia kila kitu lakini haijawahi kuwa Big issue huko State.
 
tatizo lao hawampendi mtu yoyote anaeshirikiana na diamond...
halafu hamornize ana sauti yake na diamond ya kwake....
kwenye masikio ya haters ndo wanasikia zinafanana...
labda mseme anaiga uimbaji...
na ukiiga uimbaji hata msipofanana sauti utaonekana unafanana.
 
Kuna Kitu cha kujua kabla ya Kumjudge mtu yeyote hapa Ulimwenguni. Sam Misago ni mwanadamu kama walivyo wanadamu wengine hapa chini ya Jua. Ana mapungufu yake na Mazuri yake pia na Kamwe hawezi kuvutia kwa asilimia Kubwa. Zaidi ya yote ni kwamba UKWELI unapo-tajwa juu ya mwanadamu awae yeyote, HUCHOMA kama maji ya moto juu ya Ngozi ya KICHANGA ni dhahiri shahir kwamba Sam Misago alimpa za USO huyu bwana mdogo Sheta na ndivyo ilivyo hata huku mtaani kwamba Sheta hana Nguvu yeyote kwenye Game kwa sasa na ndio maana Alikosa raha wakati akifanyiwa Interview sababu alifahamu kwamba Mfalme sasa kapigwa na Yuko teyari Kupelekwa utumwani pamoja na watu wake kwa kipindi cha Miaka 20.
 
Watz tumezidi lawama hv fnl na hawa shilawadu kina nani wanabore mambo yao? au kwakuwa wanaelekea kwenye ugawaji wa tuzo ? tubadilike bana kwenye ukweli tuambizane ukweli
chilawadu wapo juu wewe shirika la wambea duniani KWETU MBEYA NAMI NI MMBEYA
 
Pole mkuu na najua familia yenu ya wasafi mmeumia kweli kweli kutokuwemo kwenye hizi tuzo wakati wenyewe mmeleta pozi kujaza fomu.

Sasa naona mmeamua kuungana ili Tuzo iende kwenye Shetta ila kwa akili ya kawaida tu Nurdin Shetta anaweza kupata Tuzo mbele ya Ali?!
 
pole nawewe..!
 
Mkuu swala la kufanana sauti plus style kwenye mziki ni kitu cha kawaida kutokea. Na ndio maana hakuna kesi iliyowahi kufunguliwa kuhusiana na hizo mambo. I bet utakua unawajua Future na Disigner(Panda) .. Hawa jamaa wanafanana karibia kila kitu lakini haijawahi kuwa Big issue huko State.

unatakiwa utumie akili tu hata ya darasa la nne,

sasa harmonize wa nini kama ladha zote na style zote anazofanya tunazipata kwa diamond?

think critically.
 
Hata the Beatles.
 
unatakiwa utumie akili tu hata ya darasa la nne,

sasa harmonize wa nini kama ladha zote na style zote anazofanya tunazipata kwa diamond?

think critically.
as long as ana mashabiki tena wengi tu hizo principles zako haziexist... Wanaomcopy Diamond nchi wengi sana. Lakini kwanini anasikika yeye tu? what's so special about him? is it only about copying? kama kufanana na Diamond kunampa mashabiki na kumletea pesa kwanini abadilike? Em jaribu kutumia elimu yako ya chuo kikuu hiyo si itakua biashara kichaa?
 
Wameona jamaa hadi alilie tuzo za nje ndio apewe,si bora tumuanzishie za hapahapa ili tumlundikie,kisha kuna mazombi yamepeleka maombi ya kuzigombea hizo tuzo,wakati wanajua kabisa zimeandaliwa ili wampe nani ............... Natamani kuwaambia wajitoe,lakini muziki wao bado mdogo kwahiyo itakula kwao kama ni jambo la kujua wasingeshiriki tu.
 
Kwani uongo Harmonize hamuigi Diamond kila kitu hadi kunyoa kiduku?
Ndio anamuiga kila kitu,na hajafunja sheria za nchi wala za burudani na si kosa popote pale duniani. Na tupo wengi tu tunaopenda anavyomuiga na ndio maana anapata pesa na maisha yake yanasonga.

Kabla "hajaiga" alikuwa ni kapuku fulani ambaye hata hapa tulikuwa hatumjui.
 
Watz tumezidi lawama hv fnl na hawa shilawadu kina nani wanabore mambo yao? au kwakuwa wanaelekea kwenye ugawaji wa tuzo ? tubadilike bana kwenye ukweli tuambizane ukweli
Wewe huongei ukweli,ila unapotosha kwa kitu unachokijua. Hebu mwenyewe sema,Sam ni mtangazaji wa TV iliyoandaa hizo tuzo hatakiwi kuwahoji wasanii kama vile wao tayari wana mtu wao,maswali yale angekuwa sio wao ndio waandaaji alikuwa sahihi,lakini wao ndio waandaaji hawatakiwi kuwahoji wasanii kwa stahili ya kama tayari wamemuandaa mtu wao.
 
Nimekuwa nikifuatilia sana hiki kipindi cha Friday Night Live kinachorushwa kila Ijumaa ya wiki usiku na Sam Misago. Kumekuwa na interview za wasanii mbalimbali lakini nimegundua hiki kipindi ni jipu kwa wasanii wetu!!!

Anachokifanya Sam ni ujinga wa hali ya juu ambao hauwezi kuvumilika! Kama kuna wadau wengine huwa wanafuatilia hiki kipindi mtakuwa mmegundua na kuona nini kinachoendelea!!

FNL ya juzi kama uliona Shetta alikuwa ana interview kwenye hicho kipindi na Sam lakini Sam alionesha kutomkubali kabisa Shetta kutokana na maswali aliyokuwa anamuulizaa! Swala la EATV Awards, Sam alionekana kumkandia sana Shetta na kuonesha waziwazi kuwa katika vipengele alivyopo Shetta ni kama hawezi kuchukua tuzo kwa sababu fulani yupo! SHAME ON U SAM!

Wewe ndiye unayeamua mshindi au kura ndo zinaamua? Na kama mnajua fulani ndo atakuwa mshindi, ya nini kuweka usiku kwanini msimpe Tuzo aendeee? Kwanini kuna mashindano?

Shetta alipoteza kabisa 'mood' juzi kutokana na Sam. Kwa walioona watakuwa mashahidi wa hayaa. Sijui ni kukosaa taaluma ya utangazaji au la, lakini hii sio maara ya kwanza kwa Sam. Nakumbuka kuna siku Harmonize alikuwa na Interview FNL, Sam alikomaa na Swala la Harmonize kumuiga Diamond hadi Harmonize akapanic maana anajibiwa lakini interview nzima ni kama alimuitia kumuuliza hilo swalii!

Sam na FNL yake sio hayoo tu, yapo mengi lakini kwa hili la juzi ni wakati wa wasanii sasa Kukisusia hiki kipindiii kwa alivyofanyiwa Shetta!!! Na kwa maswali yale, ningemuomba Shetta kiutu uzimaa ajitoe kabisa katika kuwania tuzo hizi za AETV awards!! Maana aliabishwa kuwa hawezi shindana na Mwafulani!!!

Sam kama upo hapa na unasoma haya au jamaa ake yeyote wa karibu amfikishie taarifa nafikiri kungekuwa kuna kupiga simu kipindi cha juzi Sam angekoma!! Utangazaji bila taaluma matokeo yake ndo hayo.

80ebefb3071dc7160357f7d185c8a5d8.jpg
Tuzo za mchangan hizo
 
Muacheni Sam aseme ukweli,mmezidi hamtaki ukweli usemwe.
Yeyote anayesema ukweli kuhusu hao WCB au wenye ukaribu nao anaoneka yupo upande wa Kiba.
Nifah ukiwa huku unajitoa akili sana,ishu sio aseme ukweli au hasiseme ukweli,hayo ni matatizo yake hayawazuii watu kushabikia wanachokishabikia,ila hoja ambayo iliyopo ni KWASABABU WAO NI WAANDAAJI WA HIZO TUZO HAWATAKIWI KUWAHOJI WASANII KAMA VILE WANAJISUMBUA KWA KUJIINGIZA KWENYE KINYANG'ANYIRO CHA TUZO ZAO.(maana alivyokuwa anamuhoji Shettah ni kama vile alikuwa anamwambia acha kujisumbua sisi tunae mshindi wetu,lakini kama ulikiangalia kile kipindi.)
 
Nikisoma katikati ya mstari kuna kitu nakiona, Sam ni mkweli, so wasema ukweli huwa wanachukiwa.
Ukweli upi sasa anaousema .......... EATV NDIO WAANDAAJI WA HIZO TUZO,HALAFU SAM ANAMUHOJI MMOJA WA WASHIRIKI KAMA VILE WAO WAANDAAJI WANA MSHINDI WAO KITU AMBACHO SI SAHIHI,ILA INGEKUWA HIZO TUZO WAO HAWAKUZIANDAA BASI YALE MASWALI ALIKUWA SAHIHI MNO NA HATA MIMI NINGEMUONA WA MAANA.
 
unatakiwa utumie akili tu hata ya darasa la nne,

sasa harmonize wa nini kama ladha zote na style zote anazofanya tunazipata kwa diamond?

think critically.
Harmonize si muhimu kwako kama ulivyo wewe si muhimu kwake,yeye anafanya Muziki kutengeneza maisha yake,na Mungu anamjalia anandesha maisha yake fresh tu,anapiga shoo angekuwa si wa umuhimu WATU WASINGEKUWA WANAINGIA KWENYE SHOO ZAKE,MAANA ZINGINE ANAPIGA PEKE YAKE NA WATU NYOMI.
 
Back
Top Bottom