Rymez40
New Member
- Mar 16, 2021
- 1
- 2
Samadi ya maji ya majumbani ni mchanganyiko wa samadi ya kuku, kinyesi cha wanyama wa kufugwa katika hali zote mbili yaan unyevu au ukavu. Wanyama hao ni ng'ombe, nguruwe, mbuzi na kondoo pamoja na maji.
Viungo vyote hivi vina changanywa kwa pamoja na vinaweka kwenye chombo kama ndoo au kuroba na kutobolewa vitundu vidogo vidogo ila kuruhusu matone ambayo yataifadhiwa katika ndoo hadi itakapo jaa.
Samadi ya maji iliyo kwenye ndoo au beseni itakorogwa polepole na kwa muda mrefu wastani wa nusu saa ili iweze kuchanganyika vizuri na hapo sana samadi ya maji itakuwa tayari kwa kuwekwa shambani au kwenye bustani.
Kwa maeneo ya mijini kilimo cha mbogamboga kinafanyika sana na bustani samadi ya maji itasaidia sana na kupunguza gharama za kununua mbolea na maeneo ya vijinini kwa wakulima wadogo wadogo hawawezi kulipia gharama zote za mbolea ya kiwandani pamoja na dawa za Kuuwa wadudu. Zifuatazo ni faidi za samadi ya maji.

- Kwanza inasaidia mimea kupata virutubisho kwa urahisi zaidi kuliko mbolea ya kiwandani au samadi za kawaida: kwa sababu samadi ya maji ipo katika hali ya kimiminika hivyo basi mimea iliyo pandwa shambani au mbogamboga zilizo bustanini itapata virutumbisho moja kwa moja yaani ikiwekwa tu hapo hapo inafanya kazi.
- Pili itapunguza gharama za kununua mbolea ya kiwandani kwani:Wakulima wadogo wadogo wote nchini wanaweza kuitengeneza hii na wakatumia na kupunguza gharama amabayo ingeletwa na kununua mbolea.
- Tatu itasaidia kuokoa muda ambao utapotea bure katika kumwagilia na kuweka mbolea: Hii samadi ya maji yenyewe ina maji na samadi kwa pamoja hivyo basi wakati wa kuiweka shambani au bustanini unaweka vyote mawili kwa pamoja.
- Nne ni rahisi kuhifadhi: Mara tu baada ya kutengeneza basi unaweza kuitumia na kama umetengeneza kwa kiwango kikubwa basi utaweka tu kwenye ndoo, jaba, beseni na hata kwenye dumu na utaweka pahala pakavu na Salama.
- Tano gharama yake ya kutengeneza ni ndogo: kwa vile gharama yake ya kuanzisha na kutengeneza ni ndogo sana hivyo basi watu wote wanao uweze wa kutengeneza hata kwa wale wakulima wadogo wadogo.
- Sita hakuna upotevu wa virutubisho: wataki inatumika basi kwa asilimia ndogo sana kama 3-5% cha upotevu wa virutubisho ndio vinaweza vikapotea na hii pisa husababishwa na kukosa umakini wakati wa kuiweka shambani.
Upvote
1