samahani naomba ufafanuzi

samahani naomba ufafanuzi

papag

JF-Expert Member
Joined
Jul 31, 2009
Posts
1,156
Reaction score
1,667
habari zenu na poleni na majukumu ya kila siku ya kujenga na kubomoa taifa hili la mdanganyika.
swali langu ni kama ifuatavyo:-
kuna misiba mingi ambayo imetokea na hao wafu kwa namna moja au nyingine wametokea kuwa maarufu ktk jamii yetu ndani na nje ya nchi lakini sijaona viongozi w serikali au chama wakiwapa kipaumbele zaidi ya maneno ya kwenye majukwaa.kwa ufupi nitawataja wale ambao wametangulia mbele za haki huku mimi nikiwa na akili ya kujua baya na zuri.
tukianzia na watu kama kina TX MOSHI wiliam sikuona shamra shamra yeyote kutoka serikalini hata kutoa ubani wa laki 2.km walitoa basi ilikuwa kimya kimya sio kwa mbwembwe za kwenye makamera.
Ukija kwa mzee docta Remmy mtoro ramadhani ongalla naye sijui km yalifanyika yeyote toka kwa serikali kwa mbwembwe na bashasha.hawa ni wachache ambao kwa kiasi kikubwa wameweza kuitangaza nchi hii ya baba wa taifa.na mwishowe kufa na kutothaminiwa kama sisi binadamu tunapofuga mbwa na siku akifa unakwenda mtupa barabarani.
Sasa swali langu ni hili hivi ni kweli kabisa hawa wazee hawajafanya la maana kuliko huyu marehemu wa juzi?yaani KANUMBA?
Samahani kama nimewakwaza ila nataka mnifahamishe au ndiyo yale yanayosemwa hawa woote ni freee.................?
nawakilisha
 
sahau wote hao..kwa sasa kuna msiba wa Gen. Ernest Kyaro. Lakini hata updates za msiba unaendeleaje hatupati! Hii ndio Tz ni zaidi ya uijuavyo.
 
Vifo vya hao marehemu havikuwa na TIJA KISIASA...........................!
 
.....Kanumba was...... "The .....!!"
Malizia mtoa mada....
 
suala la muda tu ... nyakati na ukaribu
 
Back
Top Bottom